Kiongozi wa Uamsho aachiwa kwa dhamana Zanzibar

HALI sasa ni shwari na kwamba shughuli za maisha zimearudi kama kawaida. Viongozi wa jeshi la polisi, wanasiasa, na wa jumuiya za kidini wamo kwenye mikutano ya kutuliza hali na kujenga tena mazingira ya kuaminiana na kufanya kazi pamoja. Akizungumza na Deutsche Welle kwa njia ya simu kutokea Zanzibar hapo jana, Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali, alisema hali …

Urussi yashutumu Syria kushambulia raia

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa yake kulaani hatua ya Serikali ya Syria kwa kufanya mashambulizi kwa kutumia Vifaru vya Kijeshi na Makombora dhidi ya Mji wa Houla. Kauli ya Urussi ikishutumu matukio nchini Syria kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kumezusha suali kama ni mabadiliko katika msimamo wa nchi hiyo kuhusu Syria. Na je …

SYRIA: vita vya wenyewe kwa wenyewe vyanukia

MKUU wa ujumbe wa umoja wa mataifa ameonya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria baada ya wachunguzi hao kuhesabu miili 92, 32 ikiwa ni ya watoto ,katikati ya mji wa Houla kufuatia ripoti za mauaji. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amejiunga na sauti za kimataifa kushutumu mauaji hayo siku ya Jumamosi , huku kukiwa na miito …

Rwanda yashutumiwa kuchochea uasi DRC

Umoja wa Mataifa umesema uasi ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unachochewa na nchi jirani ya Rwanda. Taarifa ya ndani ya umoja huo ambayo BBC imeiona, inaishutumu Rwanda kwa kuwapatia silaha na askari waasi wa Congo. Taarifa hiyo imezingatia mahojiano na waasi ambao wanasema waliandikishwa Rwanda kwa kisingizio cha kujiunga na jeshi la nchi hiyo, lakini walipewa silaha …

mwendesha mashtaka mkuu wa ICC

ICC”Viongozi wa Afrika msitishike na wababe wa kivita”

MWENDESHA mashtaka mkuu mpya katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Fatou Bensouda, amesema wababe wa kivita wanawatisha viongozi wanaojaribu kuwatia mbaroni. Bi Bensouda ametoa wito kwa viongozi wa Afrika wasikubali kutishwa na viongozi kama vile jenerali muasi Bosco Ntaganda. Jenerali Ntaganda anakabiliwa na tuhuma za uhalifu wa kivita na kwa kuwasajili watoto vitani huko Jamhuri ya Kidemokrasia …

Hakuna dalili ya makubaliano Iran na IAEA

MAZUNGUMZO baina ya Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki IAEA Yukia Amano na Viongozi wa Iran, kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo hayajaonyesha dalili ya kufikia makubaliano. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki IAEA Yukia Amano, amefanya mazungumzo na Iran juu ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo ambao umegubikwa na utata. Mazungumzo …