Mapigano yazuka Mashariki mwa DRC

MAPIGANO makali yamezuka tena Mashariki mwa Jamhuri ya Kideomkrasi ya Congo DRC kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa M23 wanaomuunga mkono mbabe wa kivita Bosco Ntaganda. Habari zinasema kuwa kundi lingine la wanamgambo kwa jina la Maji maji linalodai kuwatetea raia limejiunga katika mapigano hayo. Raia wanazidi kuyakimbia makaazi yao hususan katika wilaya ya Masisi katika mkoa wa …

Waasi wadhibiti uwanja wa ndege Libya

KUNDI moja la wapiganaji wakiwa silaha kali wamedhibiti barabara ya ndege katika uwanja wa ndege jiji kuu la Tripoli, Libya. Waasi hao wamekuwa wakitaka kuachiliwa kwa kiongozi wao wanaodai alikamatwa Ijumaa wiki jana. Kundi hilo la al-Awfia brigade liliingia katika uwanja wa ndege hali iliyolazimisha ndege nyingi kubadilisha safari. Haijabainika ikiwa kiongozi wa kundi hilo anazuiliwa na serikali ili kuhojiwa. …

Ajali ya ndege Nigeria 150 watoweka

Ma afisa wa Nigeria wanasema kuwa ndege ya abiria imeanguka kwenye eneo la makaazi mengi, katika mji mkubwa kabisa wa nchi, Lagos. Walioshuhudia tukio hilo wanasema waliona ndege ikigonga jengo na kuwaka moto. Ndege ilikuwa imebeba kama mia-moja-na-50. Haijulikani wangapi wamenusurika. Mkuu wa Idara inayoshughulika na safari za ndege, Harold Denuren, alisema ndege hiyo ilikuwa inatoka Lagos, kusini mwa Nigeria, …

Malkia ahitimisha sherehe za miaka 60

ZAIDI ya watu milioni moja waliohimili mvua kali wameshuhudia msafara wa Malkia wa takriban mashua 1,000 wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya utawala wake kupitia mto Thames. Mashua ya Malkia ilikua katikati ya msafara wa mashua za aina mbalimbali, zinazotumia nishati ya mvuke, za kupiga kasia, mashua za kifahari, kayak na mjengo wa Kichina maarufu kama Dragon. Shughuli hii ni …

Zaidi ya Watoto elfu 40 waasiliwa

Shirika la kuteteta maslahi ya watoto la The African Child Policy Forum linasema zaidi ya watoto elfu 40 wameasiliwa katika kipindi cha miaka minane wengi wakiwa na walezi kutoka Marekani, Ulaya Magharibi na Canada. Watoto wengi hasa wanaasiliwa kutoka Ethiopia ambayo inatuma watoto wengi ugenini nyuma ya China. Kuna zaidi ya mashirika 70 yanayoshughulika na mpango wa kuwaasili watoto nchini …

Charles Taylor miaka 50 jela

RAIS wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na Makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita. Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002. Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana …