KENYA imetangaza siku tatu za maombolezi baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya, Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Bwana Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu, kujadili tukio …
Maharamia kushtakiwa Mauritious
UINGEREZA imetia saini mkataba na Mauritious kuruhusu washukiwa wa uharamia waliokamatwa na jeshi na wanamaji kupelekwa kisiwani humo kwa mashtaka. Waziri mkuu David Cameron alikutana na mwenzake wa Mauritious Navin Ramgoolam nchini Uingereza kwa makubaliano hayo. Cameron ameutaja mkataba huo kama hatua muhimu katika vita dhidi ya maharamia sugu wanaoendesha harakati zao katika upembe wa Afrika. Makubaliano sawa na hayo …
Rais Omar El Bashir kikwazo Malawi
SERIKALI ya Malawi, haitakuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Afrika uliotarajiwa kufanyika mjini Lilongwe mwezi Ujao. Hatua hii imekuja baada ya malumbano kuhusu rais wa Sudan Omar El Bashir anayetakiwa na mahakama ya ICC kwa makosa ya Jinai ikiwa aruhusiwe au asiruhusiwa kuhudhuria mkutano huo. Umoja wa Afrika ulikuwa umesisitiza kuwa lazima Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, aalikwe. Muungano …
IMF kurejesha ufadhili kwa Malawi
SHIRIKA la Fedha Duniani IMF limesema kwamba litatoa dola milioni 157 kama mkopo kwa Malawi ili kuuchepua uchumi wake ambao umedorora.Malawi imekuwa na matatizo ya uchumi wake tangu IMF kukatiza ufadhili wake mwaka jana. Rais wa zamani Bingu wa Mutharika ambaye alifariki dunia hapo mwezi Aprili alikosolewa vikali na jamii ya kimataifa kwa ukiukaji wa haki za binadamu pamoja na …
Mshirika wa Gbagbo akamatwa.
RAIS wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na Mkewe Simone Mshirika mkuu wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amekamatwa nchini Togo na kurudishwa nyumbani. Moise Lida Kouassi ni wa kwanza kati ya washirika wa Bwana Gbagbo kukamatwa kwa kuhusika na mgogoro wa mwaka jana uliofuatia uchaguzi wa mwaka 2010. Hali hiyo ilifuatiwa na mvutano wa miezi minne …
Mamilioni kwa watakaowafichua al-shabaab
SERIKALI ya Marekani imetenga dola milioni 33 kwa watakaotoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa viongozi saba wa kundi la al-shabab nchini Somalia. Marekani na wachambuzi wengine wa masuala ya usalama wamehusisha kundi hilo na lile la al Qaeda. Viongozi hao ni pamoja na kiongozi mkuu zaidi Mohamed Abdi aw-Mohamed, maarufu Sheikh Mukhtar Abu Zubeyr au jina lingine Ina Gudane yaani mtoto …