Al-Shabab wajisalimisha

Kundi la wanamgambo nchini Somalia lenye uhusiano na Al-Qaeda ,Al-Shabab, linaonekana kuishiwa nguvu kabisa kwani baadhi ya wanamgambo hao wanaamua kujitoa na kurejea katika maisha ya kawaida. Abshiri Ali Mohamed ni miongoni mwa wanamgambo waliokuwa ni tishio katika pembe ya Afrika ambapo ni mafanikio yanatokana na Majeshi ya Afrika kuwafurusha majuma ya hivi karibuni. Hasa katika miji ya Elasha Biyana …

Uamuzi wa mahakama Misri wazua wasiwasi

UAMUZI wa mahakama uliotolewa siku mbili kabla ya kufanyika duru ya pili ya kinyang’anyiro cha urais, unalipa baraza la utawala wa kijeshi nguvu za bunge. Wanaharakati na wanasiasa wamelishutumu jeshi kwa kufanya mapinduzi. Kulingana na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, uamuzi huo una athari kubwa hasa kwa kuwa umetolewa kabla ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi mwishoni mwa …

Tanzania yamkamata Erdogan

MTU mmoja anayeshukiwa kuwa ana uhusiano na shambulio la mwezi uliopita katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi amekamatwa nchini Tanzania. Polisi ya Kenya inasema kuwa Emrah Erdogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki. Kenya inadai kuwa alivuka mpaka mapema mwezi Mayi kutoka Somalia ambako alishiriki mapigano kwa niaba ya kundi la Al Shabab. Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa …

Sheria ya ndoa za jinsia moja Uingereza

KANISA la Kianglikana la nchini Uingereza limepinga vikali mpango wa serikali wa kutaka kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja. Taarifa rasmi ya kanisa hilo imesema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa imeleta mgawanyiko na ni yenye mapungufu -na inayotishia kuleta Uhasama mkubwa baina ya Kanisa na Serikali. Ikitoa jibu lake kuhusiana na swala hilo nchini Uingereza na Wales, kanisa imesema kuwa …

Odinga ataka EU kuwashambulia al-shabab

WAZIRI Mkuu wa Kenya Raila Odinga ameomba msaada kifedha na vikosi kutoka Marekani na Ulaya kuwatoa al-Shabab kwa ‘shambulio la mwisho’ katika mji wenye bandari wa Kismayo. Raila Odinga alisema vikosi vyaKenya vinatarajia kuingia Kismayo mwezi Agosti na alisema al-Shabab itahitaji “operesheni ya kivita ardhini, baharini na angani”. Lakini msemaji wa sera za nje wa Muungano wa Ulaya Michael Mann …

Wakili wa ICC akamatwa Libya

Wakili wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, amekamatwa nchini Libya, akishutumiwa kuwa alimpa Seif al-Islam – mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Wakili huyo, Melinda Taylor, amezuwiliwa katika mji wa Zintan, magharibi mwa Libya, ambako alikwenda kumhoji Seif al-Islam kwa ruhusa ya wakuu wa Libya. Seif al-Islam anakabili mashtaka na ICC na wakuu wa Libya, kwa yale …