Taliban washambulia hoteli Kabul

Wanamgambo wa kundi la Taliban waliojihami na silaha wamevamia hoteli mmoja mjini Kabul na kuzua mapambano makali na vikosi vya usalama nchini Afghanistan. Visa vya ghasia vimeongezeka nchini Afghanistan Maafisa wa usalama wanasema wanamgambo hao waliokuwa wamejihami na maguruneti na bunduki za rashasha walivamia hoteli ya Spozhmai ilioko kando kando ya ziwa Qargha. Yamkini watu wawili wamefariki na wengine wakiwemo …

Sheria ya kutotoka nje yatangazwa Nigeria

Maafisa wa Nigeria wametangaza sheria ya kutotoka nje katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Damaturu kufuatia makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa kisiilamu na pia sheria hiyo imerejeshwa tena katika jimbo la Kaduna. Makabiliano kati ya jeshi na wapiganaji wa kiisilamu eneo la Damaturu yalianza Jumatatu, siku moja baada ya kutokea mashambulio ya mabomu yaliyolenga makanisa jimbo la …

Wawili waachiliwa na maharamia Somalia

Raia wawili wa Afrika Kusini ambao wamekuwa wakishikiliwa mateka na Maharamia wa Kisomali wameachiliwa huru. Wawili hao, Bi Calitz na Bwana Pelizzari, ambao ni mtu na mkewe wamekuwa wakizuiliwa nchini Somalia kwa miezi 20. Taarifa zinazohusiana Waziri wa ulinzi wa Somalia amesema jeshi na walinda usalama walikuwa wameanza harakati za kuwaokoa watu hao siku ya Jumatano usiku. Bi Calitz na …

Afungwa maisha kwa kumuua Malkia

Mahakama ya kimataifa inayochunguza mauji ya kimbari nchini Rwanda{ICTR} imemhukumu mwanajeshi wa zamani kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na mauaji hayo ya mwaka 1994. Ildephonse Nizeyimana,alipatikana na hatia ya kuamrisha mauaji ya aliyekuwa Malkia wa jamii ya Tutsi Rosalie Gicanda pamoja na mauaji mengine.Nizeyimana alikamatwa nchini Uganda mwaka wa 2009. Aliongoza kitengo cha ujasusi na operesheni za jeshi katika …

Mubarak taabani

TAARIFA za kutatanisha zimeibuka kuhusu afya ya Hosni Mubarak aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano ya kutaka mageuzi nchini Misri mwaka jana. Baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa uhai wake unasitiriwa kwa kutumia mashine baada ya kuhamishwa kutoka gerezani hadi kwenye hospitali ya kijeshi mjini Cairo. Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela Mubarak mwenye umri wa miaka 84 aliugua kiharusi …

Gambia yajivunia Bi Fatou Bensouda,

Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya kukabiliana na Uhalifu wa Kivita ameapishwa mjini Hague hii leo. Bi Fatou Bensouda, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Haki nchini Gambia,ndiye Mwafrika na pia mwanamke wa kwanza kushikilia cheo hicho. Mojawapo wa wajibu wake wa mwanzo ni kumleta Hague mwana wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gadaffi, ambaye …