UMOJA wa Mataifa umeelezea wasi wasi dhidi ya usalama wa mji wa kale wa Timbuktu kaskazini mwa Mali huku machafuko yakiendelea eneo hilo. Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni{UNESCO} limesema Timbuktu na kaburi la Askia ambalo limekuwepo tangu karne ya 17 katika mji wa Gao ni maeneo yanayokumbwa na hatari. Makundi ya Kiisilamu yameuteka mji wa Gao …
Majeshi ya Kiislamu yateka mji nchini Mali
MAJESHI ya Kiislam yanayohusishwa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda yameteka mji muhimu wa Gao, Kaskazini mwa Mali, baada ya siku moja ya mapigano makali dhidi ya mahasimu wao wa kikundi cha Tuareg. Msemaji wa Tuareg amesema kiongozi wao wa kisiasa amejeruhiwa katika mapigano hayo siku ya Jumanne, na amepelekwa nchi jirani kwa matibabu. Wakazi katika mji huo wamesema …
Washindi blogi bora Deutsche Welle wazawadiwa
WASHINDI wa tuzo ya mwaka huu ya Blogi inayotolewa na Deutsche Welle-The BOBs, wamekabidhiwa zawadi yao katika kongamano la vyombo vya habari-Global Media Forum mjini Bonn. “Mnawapatia sauti jamii ya wachache na mnajiwapatia uhuru wa kuzungumza.Hii ni changamoto kubwa. Deutsche Welle inataka kuonyesha umuhimu wa kazi yenu na kukupeni moyo muendelee. Mnafanya kazi ya maana.” Hayo ndio matamshi yaliyotolewa na …
Mursi rais mpya Misri
MAELFU ya wafuasi wake wanaendelea kushangiria kwenye uwanja maarufu wa Tahrir, ambako wamekusanyika tangu juzi kushinikiza kutangazwa kwa matokeo. Mursi, mhadhiri wa chuo kikuu amemshinda waziri mkuu wa zamani wa enzi za Hosni Mubarak, Ahmed Shafiq, ambaye hapo Alhamis wafuasi wake walitangaza kuwa ndiye mshindi. Mursi sasa anakabiliwa na kazi ngumu ya kupatanisha tafauti za kimtazamo na kimadaraka kati ya …
Mohammed Mursi atangazwa mshindi wa urais Misri
MURSI ameshinda kura kwa asilimia 51.7 akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya Uchaguzi wa juu wa Rais. Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika. Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako …
Marekani yazuia ripoti kuhusu uasi DRC
MAREKANI yazuia kutolewa kwa ripoti muhimu kuhusiana na waasi wanaoongozwa na Jenerali wa jeshi anayesakwa na Mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kutetetea haki za binadamu Human Rights Watch. Shirika hilo limesema Marekani imekuwa ikipinga kutolewa kwa ripoti ya harakati za waasi wanaoongozwa na Bosco Ntaganda Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. …