Waisilamu kulinda makanisa Kenya

VIONGOZI wa Kiislamu nchini Kenya wamekubaliana kuunda makundi ya kutoa ulinzi kulinda makanisa kutokana na mashambulizi kama yaliyotokea Kaskazini mwa Kenya siku ya Jumapili. Watu 15 waliuawa katika mashambulizi mawili dhidi ya makanisa mawili mjini Garissa karibu na mpaka wa Somalia. Eneo la mpakani mwa Kenya na Somalia limekumbwa na hali ya wasiwasi tangu Kenya ilipopeleka majeshi yake kupambana wanamgambo …

Hali ya wasiwasi yaibuka tena nchini Kenya

HALI ya wasiwasi imetanda nchini Kenya kufuatia vifo vya watu 17 na wengine 60 kujeruhiwa mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotekelezwa katika makanisa mawili mjini Garissa hapo jana. Ni tukio ambalo limezua hofu miongoni mwa raia kote nchini. Huku usalama ukiimarishwa katika sehemu za miji, maafisa zaidi wa usalama wamepelekwa mjini Garissa kuwasaka magaidi waliotekeleza mashambuliz hayo yaliyotekelezwa sambamba katika Kanisa …

Makundi ya kiislamu yaliyumbisha bara la Afrika

MATUKIO ya kusikitisha kwamba wanamgambo wa kiislamu wameyaharibu maeneo ya makumbusho ya utamaduni katika mji wa Timbuktu nchini Mali. Inatia wasiwawasi kwa kuwa hatua ya wananamgambo hao haihusiani tu na utamaduni, bali pia inalenga kuliyumbisha kabisa bara zima la Afrika – sababu ya kutosha kuilazimu jumuiya ya kimataifa kukabiliana na hofu mpya ya mashambulizi ya kigaidi. Ni ishara ya onyo …

Wafanyakazi wa Norwegian Refugee Council watekwa Kenya

POLISI nchini Kenya wamesema kuwa wafanyikazi sita wa shirika la kutoa misaada kwa wakimbizi wametekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Ifo ilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Dadaab kambi hiyo inatoa hifadhi wakimbizi nusu milioni Waliotekwa ni wafanyikazi wa shirika la Norwegian Refugee Council, ambalo linatoa huduma kwa wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi kwenye kambi hiyo. Taarifa zinazohusiana Kenya Msemaji …

Dawa mpya kwa wagonjwa wa Ukimwi

HUENDA wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya nchini Marekani. Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha wanafuata maagizo ya madaktari wao. Ukimwi hauna tiba lakini watafiti …

Ufadhili wa silaha waleta vita S Sudan

SILAHA kutoka China, Ukraine na Sudan zinachangia machafuko Sudan Kusini. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, Amnesty International. Ripoti ya shirika hilo imesema raia wameendelea kuawa na kujeruhiwa kiholela kwenye makabiliano kati ya kundi moja la waasi na jeshi la Sudan Kusini. Amnesty International inasema silaha kutoka Sudan, mabomu ya kutegwa arthini kutoka China na …