Dlamini – Zuma ampiku Ping Addis Ababa

NKOSAZANA Dlamini-Zuma, kutoka Afrika Kusini, ameshinda uchaguzi mkali kuwa kiongozi mpya wa Tume ya Muungano wa Afrika. Bi Nkosazana Dlamini-Zuma, alimshinda kiongozi wa Tume hiyo anayeondoka Jean Ping wa Gabon, katika uchaguzi mkali uliopigwa mara kadhaa. “hivi sasa tunaye kiongozi wa Tume ya Muungano wa Afrika Madam Zuma, ambaye sasa ataongoza siku za usoni za taasisi hii,” ndivyo alivyosema Rais …

Marekani kuibana Iran kiuchumi.

MAREKANI imewawekea vikwazo zaidi raia wa Iran na kampuni ambazo zinaaaminiwa kuwa zinachangia kwa kiasi kikubwa mikakati ya serikali ya Iran ya kuunda zana za nuklia. Wizara ya Fedha ya Marekani imesema imekuwa ikiziorodhesha kampuni kadha na watu binafsi kwa kuchangia kile ilichokitaja kuwa jitihada za Iran kuunda silaha za nyuklia. Marekani pia imesema imezitambua benki kadhaa na benki ambazo …

Waasi Congo washambuliwa na UN.

NDEGE za kivita za umoja wa mataifa, zimewafyatulia risasi waasi mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Afisa mmoja wa umoja wa mataifa amesema shambulio hilo dhidi ya waasi wa M23 limetokea kaskazini mwa Goma karibu na mpaka wa nchi hiyo na Rwanda. Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imeishutumu Rwanda kwa kusaidia waasi wa kundi la M23 …

Thomas Lubanga wa DRC ahukumiwa kwenda jela miaka 14

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemhukumu kwenda jela miaka 14, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa ‘Union of Congolese Patriots’ la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Thomas Lubanga. Hakimu Adrian Fulford aliitangaza hukumu ya Lubanga na kueleza kwamba mshtakiwa huyo atakwenda jela kwa miaka 8 tu kwa sababu ameshakaa rumande tangu mwaka 2006. Lubanga mwenye umri …

Mwaka mmoja wa uhuru wa Sudan Kusini

UMETIMIA mwaka mmoja tangu Sudan Kusini ijitangaze kuwa taifa huru. Kuanzia saa sita za usiku, raia wa nchi hiyo wamekuwa wakisherehekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba. Shamrashamra za maadhimisho ya mwaka mmoja wa uhuru zilianzia leo usiku katika mji wa Juba. Watu walikuwa wakiimba na kucheza katika mitaa ya mji huo huku wengine wakipiga honi za magari yao …

Wajua kuwa sasa unaweza kujipima UKIMWI nyumbani kwako?

MAREKANI imetangaza kuruhusu kuuzwa kwa chombo cha kupima virusi vinavyosababisha UKIMWI kwa binadamu vya HIV. Baada ya kifaa hicho maalumu cha vipimo kukubalika na kuruhusiwa mtu anaweza kujipima UKIMWI mwenyewe akiwa nyumbani. Chombo hicho ambacho sawa na kijisanduku kidogo kitamsaidia mtu kujipima wenyewe virusi vya HIV nyumbani bila msaada wa mtaalamu wa afya. Badala ya utaratibu wa sasa wa kwenda …