Waisraeli wauawa Bulgaria

Waziri wa mambo ya ndani wa Bulgaria amesema watalii watano wa Israel waliuawa kutokana na shambulio la kujitoa mhanga Waisrael hao walishambuliwa ndani ya basi katika mji wa Burgas nchini Bulgaria. Katika shambulio hilo dereva wa basi aliekuwa raia wa Bulgaria pia aliangamia. Waziri wa mambo ya ndani wa Bulgaria Tsevetanov amearifu kwamba mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliekuwa amevaa nguo …

Urusi, China zalipigia kura ya veto azimio juu ya Syria

Urusi na China kwa pamoja zimelipigia kura ya veto azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kutumika kwa Ibara ya Saba ya Mkataba wa Umoja huo kuichukulia hatua kali Syria na kusitisha umwagaji damu. Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, na msuluhishi wa kimataifa, Kofi Annan, wamezitaka nchi wanachanma wa Baraza la Usalama la Umoja wa …

Assad “huenda akatumia zana za kemikali”

AFISA mkuu kabisa kujiondoa katika serikali ya rais wa Syria, Bashar al Assad, ameambia BBC kuwa utawala wa Assad hautahofia kutumia zana za kemikali ikiona tisho kubwa dhidi yake kutoka kwa upinzani. Nawaf Fares, balozi wa zamani wa Syria nchini Iraq, alisema kuwa taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa huenda zana hizo tayari zimetumiwa. Aliongeza kuwa mashambulizi ya mabomu ambayo yameshuhudiwa …

Dunia yaadhimisha miaka 94 ya Mandela

RAIS wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo anatimiza miaka 94 tangu alipozaliwa. Siku ya kuzaliwa kwake pia inaadhimishwa na Umoja wa Mataifa kutokana na mchango wake katika kuikomboa Afrika Kusini dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi. Na nchini Afrika Kusini kwenyewe Nelson Mandela, ataadhimisha siku hii na familia yake na Marafiki huku shughuli mbalimbali zikiandaliwa nchini …

Umoja wa Afrika umepata kiongozi wa kike

Waziri wa mambo ya ndani wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini Zuma amechaguliwa kuwa Kiongozi wa kwanza mwanamke wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, AU. Uteuzi huo umemaliza mkwamo katika kinyang’anyiro cha uongozi ambao ulikuwa umetishia kuugawanya na kuudhoofisha Umoja huo. Kulikuwa na shangwe katika makao makuu ya Umoja wa Afrika – AU mjini Addis Ababa, Ethiopia baada ya Nkosazana …

Mashujaa wa Kenya mahakamani London

OMBI la raia wanne mashujaa wa uhuru wa Kenya kutaka kukubaliwa kufungua kesi dhidi ya wakoloni wa Uingereza limeanza kusikilizwa katika mahakama kuu ya Uingereza London. Wanne hao ni pamoja na Paulo Nzilu, Wambugu wa Nyingi, Jane Muthoni Mara na jamii ya Susan Ngondi. Mashujaa hao wa uhuru wa Kenya wanasema serikali ya Uingereza sharti ikiri kwamba maafisa wake walitekeleza …