Sudan yakataa makubaliano na Sudan ya Kusini
HATUA hiyo ya kutupilia mbali mpango huo uliopendekezwa na Sudan Kusini inachukuliwa wakati huu ambapo muda wa mwisho uliotolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika kwa nchi hizo kumaliza tofauti zake unakaribia kutumia. Rais Omar al-Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini. Vyombo hivyo vilizipa Sudan na jirani yake muda wa hadi …
Rais wa Ghana John Attah Mills afariki
Rais wa Ghana John Atta Mills amefariki ghafla wakati akipata matibabu. Taarifa kutoka Ofisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku. Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo. Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais. Rais Attah Mills ambaye husafiri …
Matajiri waficha fedha ng’ambo
UTAFITI mpya uliofanywa sehemu mbali mbali za dunia, kutaka kujua wapi watu wanaficha fedha zao kukimbia kodi, umegundua kuwa dola kama trilioni 20, zimefichwa nchi za ng’ambo, mbali ya macho ya maafisa wanaotoza kodi. Ripoti hiyo imeandikwa na shirika la utetezi, Tax Justice Network, ambayo inasema kuwa tofauti baina ya matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivofikiriwa. Dola trilioni 21 …
Watu 10 wamekufa katika mafuriko Beijing
Mji Mkuu wa Uchina, Beijing, umepata mvua kubwa kabisa kuwahi kutokea kwa zaidi ya miaka 60. Watu wapatao 10 wamekufa, na maelfu wamehamishwa makwao. Mvua kubwa ilifurika mabara-barani, kupeperusha mapaa, na kuporomosha miti na milingoti ya taa. Maji mjini yalikuwa yanafika kiunoni. Safari za ndege zaidi ya mia mbili zilivunjwa, na hivo kuwaacha maelfu ya watu wamenasa kwenye viwanja vya …