Mitt Romney Amwita Mgombea Trump ‘Tapeli’

ALIYEKUWA mgombea wa urais kupitia Chama cha Republican nchini Marekani, Mitt Romney ameibuka na kukitaka chama chake kutomteuwa Donald Trump huku akimtaja mgombea huyo aliyeshinda kuwa ni tapeli. Romney ametoa shutuma hizo kwa Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari. Trump hatahivyo amemkejeli Romney katika mtandao wa tweeter kama mgombea …

Kesi ya Ingabire Yatua Mahakama ya Afrika

Na Kulwa Mayombi, EANA Kesi ya mwanasiasa mfungwa raia wa Rwanda,Bibi Victoire ingabire (42), kusikilizwa katika mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu jijini Arusha Ijumaa, Machi 4 2016. Ingabire analalamika kuvunjiwa haki zake za msingi za binadamu na haki katika mchakato wa usikilizishwaji kesi yake nchini Rwanda kama ilivyoainishwa katika mkataba wa …

Biashara Ikupasayo Kufanya ni Ipi?

Na; Joseph Mayagila, AJTC Kwanini unapanga kufanya biashara hiyo? Au Kwanini unafanya biashara hiyo unayoifanya? Je ulikuwa umepanga kufanya biashara hiyo au umejikuta tu unafanya biashara hiyo kwasababu ya ugumu wa maisha au kwasababu huna namna nyingine? Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha watu kufanya biashara wanazofanya. Ila katika kanuni za uchumi, ni vema unapochagua biashara uzingatie vigezo vifuatavyo: Kigezo cha kwanza …

Mpinzani wa Museven, Besigye Aeleza Alivyovyanyaswa na Polisi

KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye ameliambia shirika moja la habari Kuwa alitiwa mbaroni na polisi nchini humo mara nne kwa muda wa siku sita kufuatia uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita. Licha ya mshikemshike alioupata matokeo ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Rais Yoweri Museven kutawala nchi hiyo kwa muhula wa tano mfululizo. Bw. Besigye ambaye yupo kizuizini nyumbani kwake kwa …

Yoweri Museveni Atangazwa Mshindi wa Urais Uganda

TUME ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa ni mshindi wa Uchaguzi wa Urais uliofanyika Alhamisi iliyopita. Kwa mujibu wa tume hiyo Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dk. Badru Kiggundu. Mpinzani wake mkuu Dk. Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia …

Boutros Boutros-Ghali

R.I.P Boutros Boutros-Ghali

RIP diplomat Boutros Ghali siku na nyakati za maisha yako UN zimeongeza nguvu katika mjadala wetu wa leo kwamba:siasa za UN ni nzito na zinawezwa na wazito kama nchi inataka kweli kujiweka ktk ramani ya dunia!