HELIKOPTA tatu za Uganda zikiwa njiani kuelekea Somalia zimepotea katika ardhi ya Kenya. Maofisa wa jeshi la Kenya wamesema kwamba helikopta nne ziliondoka Uganda na moja ikatuwa mjini Garissa. Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Kenya, Bogita Ongeri, helikopta hizo zilipotea karibu na eneo la Mlima Kenya, lakini rubani mmoja aliweza kuwasiliana nao, akiomba msaada. Kwa mujibu wa msemaji …
Bolt na Rudisha waendelea kutesa Olimpiki
MKIMBIAJI wa kasi duniani kwa sasa ni Usain Bolt ambaye ametimka mbio na kufanikiwa kutetea taji lake la mbio za mita 200 katika michezo ya Olimpiki akiongeza mavuno ya nchi yake Jamaica ya medali za dhahabu. Usain Bolt amekuwa pia mtu wa kwanza duniani kuweza kushinda mbio za mita 100 na 200 katika msimu mmoja wa Olimpiki. Lakini la kusisimua …
OXFAM yahudhunishwa na vita vya Congo, DRC
VIONGOZI wa mataifa 11 ya eneo la Maziwa Makuu wanatarajiwa kukutana mjini Kampala Uganda kwa kikao cha dharura kutafuta suluhu la mzozo wa kivita unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Rwanda inashutumiwa kuwasadia waasi wa kundi la M 23 wanaopigana na vikosi vya Serikali, shutuma ambazo inapinga vikali. Wakati huo huo shirika la Oxfam linasema mamilioni ya …
Clinton azipongeza serikali za Sudan kumaliza mzozo
VIONGOZI nchini Marekani na Ulaya wamesifu makubaliano yaliyofikiwa Agasti 04, 2012 kati ya Sudan na Sudan Kusini kumaliza mzozo wa mafuta, ambao umesababisha matokeo mabaya ya kiuchumi na kutishia vita. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Hillary Rodham Clinton , ambaye amefanya ziara Sudan ya Kusini kama sehemu ya ziara yake katika bara la Afrika, alitoa sifa hizo kwa …
Viongozi Somalia wapitisha Katiba Mpya
VIONGOZI nchini Somalia wanaokutana Mjini Mogadishu kwa wingi wameipitisha Katiba Mpya ya nchi hiyo kitendo ambacho kimefungua njia kwa Serikali mpya kuchaguliwa mwezi huu. Kura hiyo imepigwa muda mfupi baada ya watu wawili kujilipua wenyewe nje ya jingo la mkutano. Chini ya mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa bunge jipya litachagua kiongozi mpya wa Somalia Agosti 20. Somalia imekuwa …
Majeshi wa Serikali, waasi yapambana kuupigania Mji wa Allepo
MAPAMBANO ya kuuwania Mji wa Allepo baina ya vikosi vya Serikali na waasi yamezidi kupamba moto huko Syria, ambapo sasa waasi wamekiteka kituo muhimu cha ukaguzi kwenye mpaka baina ya nchi hiyo na Uturuki. Kufuatia hali hiyo, Ufaransa imetangaza kutaka kuitisha kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Waasi wamekitwaa kituo hicho cha Anadan kilichopo kaskazini magharibi mwa …