ATHARI za ghasia za Tana River hali ya taharuki inaendelea kutanda katika eneo la Tana Delta Pwani ya Kenya ambako Polisi wanasema wamegundua makaburi mawili ya siri. Idadi ya maiti waliozikwa kwenye makaburi hayo yaliyogunduliwa katika kijiji cha Ozhi ambacho kimekuwa kitovu cha ghasia hizo,haijulikani kulingana na polisi wala haijutambulishwa. Kwa sasa polisi wameomba idhini ya mahakama kuweza kufukua makaburi …
Rais Mpya wa Somalia Atawazwa
Rais mpya wa Somalia atawazwa RAIS mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, ametawazwa rasmi kwenye sherehe iliyofanywa mjini Mogadishu. Kiongozi huyo mpya, ambaye alinusurika na jaribio la kumuuwa Jumatano, alisema mambo muhimu kwake ni usalama na mapatano. Viongozi kadha wa kanda walihudhuria sherehe hiyo pamoja na waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, na rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh. …
Ziara ya Papa Benedict 16 nchini Lebanon
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Benedict 16, amewataka Wakristo na Waislamu katika Mashariki ya Kati kuunda jamii iliyostawi ya watu wa dini zote ambapo utu wa kila mtu na haki ya kuabudu kwa amani itahakikishwa. Papa alikuwa akizungumza na Viongozi wa kisiasa na kidini, katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu nchini Lebanon. Kiongozi huyo wa …
Muingereza akamatwa Uganda kwa Ushoga
MSANII moja toka Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa madai ya kuandaa na kuonesha mchezo wa kuigiza kuhusu ushuga. Taarifa kutoka Uganda zinasema Muingereza huyo alionesha mchezo huo wa kuigiza licha ya kwamba Uganda ilipiga marufuku kwa muda onesho hilo. Mtayarishi David Cecil wa Uingereza alifikishwa katika mahakama moja mjini Kampala na kushitakiwa kwa madia ya kukaidi na kupuuza amri ya …
Rais Somalia Anusurika Kuuwawa, Balozi wa Marekani Auawa Libya
RAIS mpya wa nchi ya Somalia Hassan Sheikh Mohamud, amenusurika jaribio la kumuua mjini Mogadishu. Milipuko miwili imetokea nje la lango la makao ya rais huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari. Taarifa zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa …
Makamu wa Rais Iraq Apinga Hukumu ya Kifo Dhidi Yake
MAKAMU wa rais wa Iraq Tareq al-Hashemi amepinga hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi yake na mahakama nchini humo jana kwa makosa ya kuhusika na kupanga mauaji na kujigamba kwamba hukumu hiyo ni kama medali kifuani mwake. Makamu huyo wa rais ambaye ni moja wa waumini wa madhehebu ya sunni wenye vyeo vya juu kabisaa katika serikali ya Iraq amewaambia waandishi …