Tuzo ya Mo Ibrahim Yakosa Mshindi Mwaka 2012

KAMATI ya kuteuwa mshindi wa tuzo ya Mo Ibrahim, ambayo hutolewa kwa viongozi wa Afrika walioonesha uongozi bora mwaka huu imekosa mshindi. Tuzo hiyo ya dola milioni 3.2 hutolewa kwa kiongozi wa Afrika aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia na ambaye aliimarisha hali ya maisha ya wananchi wake na kisha kuondoka ofisini kwa khiari. Kamati iliyokutana kumteua mshindi iliafikiana kuwa hakuna …

Wanawake Sasa Ruksa Kurithi Mali Botswana

MAHAKAMA Kuu nchini Botswana imebatilisha sheria ya kitamaduni ambayo awali iliwazuia wanawake kurithi mali nyumbani. Kutolewa na uamuzi huo ni neema kwa wanawake nchini humo kwani sasa wataruhusiwa kurithi mali kutoka katika familia zao. Mahakama imesema kuwa kanuni hiyo ya kitamaduni inakiuka sheria ya katiba inayosisitiza usawa kwa wanaume na wanawake. Taarifa zaidi zinasema, Edith Mmusi na dadake zake watatu …

Bara la Afrika Lafanikiwa Kupambana na Njaa

BARA la Afrika limekuwa na mafanikio makubwa katika kupambana na njaa kuliko nchi zingine katika Bara la Asia katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita. Hali hiyo imeonekana baada ya kutolewa kwa ripoti kuhusu uzalishaji wa chakula duniani. Taarifa zaidi zinasema uhaba wa chakula pamoja na utapia mlo vimepungua katika nchi nyingi barani Afrika, kulingana na ripoti hiyo inayotathmini viwango vya …

Rais Kibaki Agoma Kuidhinisha Marupurupu Manono kwa Wabunge, Asema ni Usaliti..!

RAIS wa Kenya, Mwai Kibaki amekataa kuidhinisha mipango ya wabunge wa taifa hilo kujipatia kitita kikubwa cha pesa kama marupurupu ya kuhudumu kama wabunge. Wabunge hao walipanga kujilipa dola alfu mia moja na kumi kila mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Taarifa zaidi kutoka Kenya zinasema Rais Kibaki amesema kuwa hatua hiyo inakiuka katiba na haiwezi kutekelezwa wakati ambapo walimu …

Waganda Waadhimisha Miaka 50 ya Uhuru

RAIA wa nchi ya Uganda leo wamekusanyika pamoja katika Uwanja wa Kololo nchini humo, kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Uganda kutoka utawala wa kikoloni wa Uingereza. Hakuna siku ilioonesha umoja wa Waganda, mshikamano na kujivunia kuwa raia wa Uganda kama leo. Hivyo ndivyo wanavyotaja baadhi ya Waganda wakiizungumzia Oktoba 9 mwaka wa 1962, ambapo ni miaka 50 tangu walipojinyakulia …

Mahakama Yaruhusu Mau Mau Kuishtaki Uingereza

MAHAKAMA nchini Uingereza imetoa maamuzi kuwa wazee watatu wa Kenya ambao waliteswa na majeshi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza wanaweza kufungua mashtaka dhidi ya Serikali ya Uingereza, na hivyo kuendelea mbele madai yao mengine ya ukatili. Maamuzi hayo yametolewa Oktoba 05, 2012 katika mahakama hiyo mjini London. Serikali ya Uingereza ambayo kwa miaka mitatu imekuwa ikiajribu kuzuia hatua zozote …