DURU za Jeshi la Guinea Bissau, Afrika Magharibi, zinaeleza kuwa watu waliokuwa na silaha wameuwawa kwenye shambulio dhidi ya kambi ya Jeshi nje ya Mji Mkuu, Bissau. Inaarifiwa kuwa mapambano hayo kati ya wavamizi na kambi ya jeshi yaliendelea kwa saa nzima. Waandishi wa habari wanasema shambulio hilo lilofanywa usiku wa manane, linazidisha wasiwasi nchini Guinea Bissau, ambako jeshi lilipindua …
Silaha za Wapiganaji wa Al Shabaab Zanaswa Puntland
SHEHENA kubwa ya silaha ambazo zilikuwa zinapelekwa nchini Somalia, zimekamatwa katika Jimbo la Puntland. Kwa mujibu wa Gavana mmoja wa jimbo hilo, Abdisamad Gallan alisema boti iliyokuwa inatoka nchini Yemen ilinaswa ikiwa imebeba mabomu ya kutega ardhini na zana zingine za kivita. Taarifa zaidi kutoka Somalia Abdisamad Gallan zinasema kuwa hii ni mojawapo ya shehena kubwa kuwahi kunaswa ikiwa na …
Mbunge Kenya Afikishwa Mahakamani kwa Uchochezi
KIONGOZI moja Mkuu wa Kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni mbunge mteule amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa kosa la uchochezi kwenye ghasia. Mbunge huyo, Sheikh Mohammad Dor anadaiwa kutamka kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani. Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo Omar Mwamnuadzi. …
Askari 10 wa Jeshi la Polisi Kenya Wajeruhiwa kwa Bomu
TAKRIBANI askari 10 wa Jeshi la Polisi Kenya wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi la guruneti. Maofisa hao wa polisi walikuwa wakiendesha msako katika nyumba moja mjini Mombasa, pwani mwa Kenya, ambako walifanikiwa kukamata silaha ikiwemo bunduki aina ya AK-47 na maguruneti mawili. Msemaji wa Jeshi la Polisi Kenya anasema kuwa huwenda wanamgambo wa Al-Shabab wamehusika na shambulizi hilo. Kenya kwa muda …
Obama Lands Punches In Rematch With Romney
A much more aggressive President Barack Obama showed up to the second presidential debate Tuesday, which at times devolved into angry crosstalk with Republican rival Mitt Romney. President Obama was under pressure to perform dramatically better at this debate—held at Hofstra University in Long Island, N.Y.—than the one held two weeks ago. Gov. Romney’s energetic performance at that first debate …
Zaidi ya wafungwa 100 Watoroka Gerezani Nchini Libya
MAOFISA wa Libya wamesema wamewakamata wafungwa 60 kati ya Wafungwa 122 waliotoroka jela katika Mji Mkuu wa Tripoli. Maofisa sasa wanadhibiti magereza kadhaa, likiwemo gereza la Al-Jadaida ambalo ni maalumu kwa wahalifu wa kawaida. Taarifa zaidi zinasema kuwa wafungwa 100 walitoroka kutoka katika jela la Al-Judaida mjini Tripoli. Wafungwa hao wanasemekana kuwa raia wa nchi mbalimbali na maofisa wanasema kuwa …