Ibrahim Kamwe Ajivua Ukatibu Mkuu TPBO

KATIBU Mkuu wa ‘Tanzania Professional Boxing Organisation’ (TPBO), Ibrahim Kamwe amejitoa  katika uongozi wa chama hicho cha ngumi kama kiongozi. Akizungumzia hatua hiyo Kamwe alisema ameamua kupumzika kufanya shughuli za TPBO na kurudi kwenye ufundishaji wa vijana na kuendelea na kampuni yake ndogo inayojulikana kama Bigright Promotion ambayo inajihusisha zaidi na utayarishaji wa matamasha na uandaaji wa mapambano ya ngumi. …

Miss Utalii Tanzania Kwenda Equatorial Guinea Kushiriki Fainali

MSHINDI wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Saidi Juma Mswaga, ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, ataondoka nchini 28-9-2013 kwenda nchini Equatorial Guinea, ambako Fainali za Dunia za Miss Tourism World 2013/14 zinafanyika Tarehe 12-10-2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Sipopo Conference Centre Malabo Equatorial Guinea. Kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewa na Fredy Njeje, …

Serengeti Fiesta Kutua Mtwara kwa Mara ya Kwanza Jumamosi

WASANII maarufu wa kizazi kipya zaidi ya Kumi tano watatoa burudani kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara na majirani zake katika tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2013 ambalo ni maarufu kwa” Tupo Pamoja, Twenzetu, Tukawinde” Ni Noma sanaa” litalofanyika katika uwanja wa Nangwanda uliopo mjini Mtwara. Burudani hiyo itakuwa kivutio tosha kwa wakazi wengi kutokana na …

Miss Ilala 2013 Atembelea M/S Tabata Jika, Atoa Msaada wa Vitabu

Miss  Ilala 2013 Doris Mollel akitia saini kitabu cha wageni katika shule ya msingi Tabata Jika wakati alipotembelea shuleni hapo na kukabidhi vitabu vya maandalizi ya mtihani wa Darasa la 7. Miss Ilala 2013 Doris Mollel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Tabata Jika baada ya kukabidhi Vitabu shule hapo. Baadhi …