Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam WADAU wa mambo ya utamaduni na michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni lililopangwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga. Mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, pichani. Hayo yamesemwa na mratibu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alipozungumza na mwandishi wa mtandao huu …
Warundi Kuchezesha Wanawake U20 Kombe la Dunia
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya miaka 20 Kanda ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji. Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Oktoba 26 na 27 mwaka huu wataongozwa …
Serikali Yabariki Tamasha la Utamaduni Handeni
Na Mwandishi Wetu, Handeni SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dk. Khalfany Haule, imebariki kufanyika kwa tamasha la utamaduni la Handeni Kwetu 2013, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani humo. Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango wenye mashiko …
Brigite Alfred Lyimo ‘Ang’ara Miss World…’Beauty With Purpose’!
Wakati warembo 131 leo wanawania taji la urembo wa Dunia (Miss World), Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred Lyimo ameng’ara kwa kushinda nafasi ya tatu katika kipengele cha Urembo wenye malengo maalum (Beauty With Purpose). Mrembo huyo amewashinda warembo 129 waliwania taji hilo ambalo ni kubwa baada ya lile la Miss World. Kilichompa ushindi mrembo huyo ni mradi wake wa …
Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jambo ‘Festival’ Laja…!
ZAIDI ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika Oktoba 23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini hapa. Mwenyekiti wa tamasha hilo, la Jambo Festival 2013, Augustine Namfua alisema kuwa, tamasha hilo ni la pili kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni kuwawezesha washiriki mbalimbali …