Shakira Atuhumiwa Kuiba Wimbo

IMEBAINIKA kuwa wimbo uliovuma wa mwimbaji wa Pop maarufu Shakira ulinakiliwa kwa njia isiyo halali kwa kazi ya mtungaji mwingine wa nyimbo. Kauli hiyo imetolewa na Jaji Alvin Hellerstein mjini New York. Jaji Hellerstein alisema toleo la wimbo “Loca” la lugha ya kihispania 2010 lilikiuka haki za umiliki za wimbo wa mwimbaji Ramon Arias Vazquez. Toleo la Ramon la “Loca” …

Ruvuma Yazinduwa Kampeni ya Bwela Kuni na Wimbo Maalum

BAADHI ya Vijana kutokea Mkoa wa Ruvuma wakishirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameandaa kampeni maalum ya kunadi fursa anuai zilizopo katika mkoa huo kupitia sanaa ya muziki kwa kuwashirikisha wasanii na vijana wenye vipaji. Kampeni hizo zilizopewa jina la ‘BWELA KUNI’ neno la lugha ya Kingoni lenye asili ya mkoa huo likiwa na maana ya ‘njoo hapa’ zitazinduliwa rasmi …

Wasanii wa Kilimanjaro Music Tour Wamfariji Afande Sele

   Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana, leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro. Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji …