Serikali Yahaidi Neema; Tuzo za Filamu 2015

SERIKALI imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na kujenga mazingira mazuri ili kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika, ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza katika tasnia ya filamu. Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa Tuzo za Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa …

Tanzania Launches Films Online And Goes Digital..!

 Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania, Johnson Lukaza akizungumza kuwashukuru wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za Kitanzania kupitia mtandao (online) hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanywa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Diodorus Kamala.  

TAFA Yaomba Ufadhili Tuzo za Filamu

Na Anitha Jonas – MAELEZO SHIRIKISHO la Filamu Tanzania laanda Tamasha la Tuzo za Filamu (TAFA) linalotarajia kufanyika Mwezi Mei 2015 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam lenye lengo la kuonyesha wachezaji filamu chipukizi wanaofanya vizuri katika tansia ya filamu nchini. Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba alipotembelewa ofisini kwake na …

COSOTA Yawanoa Wasanii na Wadau Juu ya Kazi Zao

CHAMA cha Kusimamia Haki Miliki kwa Wasanii na Kazi za Sanaa (COSOTA) kimekutanisha wanachama wake na wadau wengine kisha kutoa semina juu ya namna bora ya kusimamia kazi zao ili ziwafaidishe zaidi kuliko wanavyofanya baadhi ya wasanii ambapo hujikuta kazi zao zinawanufaisha wengine. Miongoni mwa mada ambazo zilitolewa kwa wanachama wa COSOTA pamoja na wadau mbalimbali ni namna ya kulinda …