mwanamuziki nyota kutoka Marekani Natalie Cole aliyetamba na nyimbo maarufu kama vile Unforgettable , amefariki akiwa na umri wa miaka 65. Mwanamuziki huyo aliyeshinda tuzo za Grammy alifariki akitibiwa katika hospitali moja mjini Los Angeles, mkesha wa Mwaka Mpya. Alikuwa amefutilia mbali matamasha kadha, ikiwemo ya mkesha wa Mwaka Mpya. Cole alipata umaarufu kama mwimbaji wa R&B kwa nyimbo kama …
Mchekeshaji Bill Cosby Atiwa Hatiani Kwa Dhuluma ya Kimapenzi
Waendesha mashtaka katika jimbo la Pennsylvania Nchini Marekani wamemfungulia mashtaka ya kwanza mchekeshaji nguli Bill Cosby . Cosby ameshtakiwa kwa makosa ya dhuluma za kimapenzi dhidi ya mfanyikazi mmoja wa chuo kikuu kimoja nchini Marekani,Kosa hilo lilifanyika mwaka wa 2004. Awali mchekeshaji huyo alikana kuwadhulumu kimapenzi akijitetea kuwa aliwahi kushiriki mapenzi baada ya kukubaliana na wanawake hao. Mashtaka dhidi yake …
Filamu ya The Force Awakens Yavunja Rekodi Ya Dunia
Filamu mpya ya Star Wars: The Force Awakens imevunja rekodi na kuwa filamu iliyozoa $1bn (£674m) kwa kasi zaidi duniani. Filamu hiyo ya JJ Abrams imefikia pesa hizo katika muda wa siku 12, na kuvunja rekodi ya awali ya siku 13 iliyowekwa na Jurassic World mwezi Juni. Lakini ingawa Jurassic World ilikuwa na nafuu ya kuonyeshwa Uchina pia, filamu ya …
Nyimbo za Christmas Zinazotamba Duniani Kwa Sasa
Katika kipindi hiki cha Sikukuu kila kona unapopita utasikia nyimbo za Chrismas zinapigwa na hata wengine kudiliki kuzihifadhi kwenye simu zao zikitumika kama milio ya kuitia. Thehabari inakuletea baadhi ya nyimbo zinazotamba kwa mwaka huu na kupendwa na watu wengi Duniani. Silent Night” – The Temptations “This Christmas” – Donny Hathaway “Someday at Christmas” – Stevie Wonder “Give Love on …
Janet Jackson Kufanyiwa Upasuaji,aahirisha ziara Zake
Mwanamuziki na nyota kutoka Marekani Janet Jackson ameahirisha ziara yake ya kimuziki ya Unbreakable ili kufanyiwa upasuaji. Jackson amesema madaktari wake wamemwambia anahitaji kufanyiwa upasuaji “haraka”.mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 49 amewambia mashabiki kupitia ujumbe mtandaoni,Hajasema anahitaji kufanyiwa upasuaji wapi na lini. Jackson alianza ziara ya Agosti mjini Vancouver na alikuwa amepangiwa kuzuru miji ya Marekani, Canada na Ulaya …