Mwanamuziki wa muziki wa Rap kutoka Marekani kwa jina maarufu Mos Def ameamrishwa kuondoka Afrika Kusini katika kipindi cha siku 14 baada ya kukamatwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji. Mos Def anayejulikana kama Yasiin Bey alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Cape Town siku ya Alhamisi baada ya kujaribu kuondoka nchini humo na stakhabadhi bandia. Idara ya maswala ya ndani …
Wasanii Watakao Wania Tuzo ya Oscar Wapatikana
Waigizaji na waelekezi wa filamu watakaopigania tuzo kuu za sanaa duniani za Oscar wametangazwa na kwa mwaka wa pili hakuna watu weusi walioteuliwa. Filamu ya The Revenant inaongoza kwa kuteuliwa kupigania tuzo nyingi kwenye tuzo hizo za 2016, ikiwa kwenye vitengo 12, huku Mad Max: Fury Road ikipigania vitengo 10. Eddie Redmayne, anayetumai kurudia ufanisi wa mwaka 2015, ameteuliwa kushindania …
Saratani Yasababisha Kifo Cha Mume wa Celine Dion
Rene Angelil, mume wa mwanamuziki mashuhuri duniani Celine Dion, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73, mwanamuziki huyo ametangaza. Bw Angelil, aliyemuoa Dion mwaka 1994 na wakajaliwa watoto watatu, amekuwa pia akihudumu kama meneja wake. Alifariki akiwa nyumbani kwao Las Vegas baada ya kuugua saratani. Dion alichukua likizo kutoka kwenye muziki kwa vipindi viwili ili kumtunza Angelil baada yake …
Filamu ya Wema ni Akiba Kuingia Sokoni
Filamu ya Wema ni akiba yake mwanamama Jennifer Mgendi imekamilika. Akiongea na blogu hii Jennifer amesema filamu hiyo ambayo imewashirikisha wasanii na watumishi mbalimbali ni stori inayomhusu kijana Mawazo anayepambana na changamoto nyingi akijaribu kulipa deni la fadhila kwa Eli alizotendewa ujanani na baba yake Eli. Fuatana naye katika filamu hii ili kupata undani wa mkasa huu.
Filamu ya Revenant imepata tuzo Kwa Ubora Wa Kuigiza
Filamu ya Revenant imepata tuzo katika hafla ya mwaka huu ya Golden Globes baada ya kushinda taji kuu la filamu yenye mchezo bora wa kuigiza. Nyota wa filamu hiyo Leonardo Di Caprio alishinda tuzo la mwigizaji bora huku Alejandro G Inarritu akishinda kwa ulekezaji bora. Filamu ya Ridley Scott,The Martian ilishinda tuzo la filamu bora ya vichekesho ikiwa ni tuzo …
David Bowie Aaga Dunia Kwa Kusumbuliwa na Saratani
Mwimbaji maarufu David Bowie, ameaga dunia akiwa na umri miaka 69, baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa saratani. Mwanawe Duncan Jones amethibitisha kifo chake na kutoa taarifa rasmi katika mitandao yake ya kijamii. Taarifa hiyo ilisema kuwa David Bowie alifariki nyumbani kwake, akiwa na familia yake. Taarifa hiyo imeelezea kuwa Bowi amekuwa akiuguza ugonjwa huo kwa muda wa …