Kundi la Musiki la ABBA Warudisha Majeshi Upya

Wanachama wote wanne wa kundi la muziki la ABBA walijumuika tena pamoja kwa sherehe ya ufunguzi wa biashara mpya mjini Stockholm. Ukumbi huo wa burudani, ambao umejengwa kwa kufuata mfano wa hoteli ya Kigiriki katika filamu ya Mamma Mia!, umetokana na wazo la nyota wa ABBA Bjorn Ulvaeus. Aliungana na wenzake Benny Andersson, Anni-Frid Lyngstad, na Agnetha Faltskog sherehe ya …

Filamu ya Star Wars Kuchelewa Kutoka, Kaa Chonjo ni Bonge La Movi

Kampuni ya Disney imetangaza kwamba filamu mpya ya Star Wars ambayo ilipangiwa kutolewa baada ya The Force Awakens itachelewa. Filamu hiyo nambari nane katika mwendelezo wa filamu za Star Wars ilipangiwa kuzinduliwa mwezi Mei 2017 lakini sasa itazinduliwa mwishoni mwa mwaka huo, sana mwezi Desemba. Filamu ya The Force Awakens, ambayo ni ya saba, ilizinduliwa mwezi uliopita na imeendelea kuvuma …

Jinsi Tuzo ya Oscar Inavyowatoa Macho Wasanii Weusi

Mcheza filamu raia wa kenya Lupita Nyong’o ameungana na wacheza filamu wengine kushutumu kutojumuishwa kwa wacheza filamu weusi au wale wachache kutoka kwa orodha ya wale wanaowania tuzo za Oscars. Katika akaunti yake ya Istagram Lupita amesema amekasirishwa sana na kukosa kujumuishwa kwa wacheza filamu weusi. Mwaka 2014 Lupita Nyong’o alishinda tuzo la Oscar kutokana na wajibu wake katika filamu …

Mwezi wa Majanga Kwa Wanamuzi, Frey Afariki Dunia

Mpiga gitaa na mtunzi wa nyimbo Glenn Frey, ambaye pia ni mwanachama mwanzilishi wa bendi ya The Eagles amefariki. Frey, amefariki jijini New York akiwa na umri wa miaka 67 baada ya kuugua wka muda. Frey alicheza na kuimba baadhi ya nyimbo maarufu zaidi za The Eagles, zikiwemo ‘Take It Easy’ na’Lyin’ Eyes’. Bendi hiyo iliunganisha mtindo wa pop, rock …

Mke Wa Will Smith Apinga Ubaguzi Wa Rangi Tuzo za Oscar

Jada Pinket mkewe nyota wa filamu Will Smith amesema hatashiriki katika tuzo za Oscar, Nyota huyo aliandika katika mtandao wake wa Tweeter mwishoni mwa wiki akionyesha kukasirishwa na ukosefu wa watu wa rangi tofauti miongoni mwa wale walioteuliwa kuwania tuzo za Oscar. Katika msururu wa ujumbe huo katika mtandao wa Twitter,Jada mwenye umri wa miaka 44 alishangazwa alipogundua kwamba hakuna …

Albamu ya Black star ya David Bowie Yaongoza Kwa Mauzo

Albamu ya Black star ya gwiji wa muziki Marehemu David Bowie inaongoza kwa mauzo nchini marekani baada ya kutolewa siku mbili kabla ya kifo chake. Albamu hiyo imeuza kopi 181,000 na hivyobasi kuipiku albamu ya Adele katika kilele cha albamu inayouza sana nchini humo. Albamu yake iliouza sana ni ile ya The Next day ambayo ilichukua nafasi ya pili kwa …