Katika maisha ya kila mwanadamu anasiku maalum ambayo hawezi kuisahau iwe ni kumbukumbu kwa jambo zuri au baya, ila bado mtu atakuwa anaikumbuka. Tarehe kama ya leo ya tarehe 28 mwezi wa kwanza mwaka 2013, ni siku ambayo mwigizaji wa Kitanzania Lulu Michael hataweza kuisahau katika maisha yake, ambapo ilikuwa siku ambayo alipata dhamana katika mahakama Kuu ya Kisitu jijini …
Chriss Brown Ashinda Kesi ya Kumpiga Mwanamke Kwenye Kasino
Muimbaji maarufu wa muziki wa kizazi kipya Chris Brown ameondolewa lawama ya wizi na kupigana na utawala wa Las Vegas Marekani baada ya mwanamke mmoja kudai alimzaba kofi na kumpokonya simu yake walipokutana kwenye Kasino moja ya kamari mapema mwezi huu. Mkuu wa sheria katika jimbo hilo Steve Wolfson amesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfungulia msanii huyo mashtaka …
Rihhana Aiachia Albamu yake Mpya ya Nane ya ANTI
Baada ya miaka minne tangu nyota wa muziki Rihhana atangaze kwamba anaandaa albamu yake mpya. Hata hivyo harakati hizo zilikabiliwa na changomoto chungu nzima na kulazimika kuchelewesha utayarishaji wake Lakini hatimaye ndoto yake imefaulu na sasa albamu hiyo ya nane kwa jina ANTI imekamilika. Nyota huyo alifanya tangazo hilo akiwa amevaa taji la dhahabu la malkia pamoja na vipaza sauti …
Wimbo Wa Adele Watazamwa Mara Bilioni You Tube
Wimbo wa mwanamuziki Mwingereza Adele umevunja rekodi nyingine kwa kutazamwa mara bilioni moja haraka zaidi katika YouTube. Video ya wimbo huo, Hello, imetazamwa mara bilioni moja katika YouTube siku 87 pekee baada ya kupakiwa kwenye mtandao huo. Wimbo huo umeupita wimbo wa Psy kwa jina Gangnam Style ambao ulitazamwa mara bilioni moja siku 158 baada ya kupakiwa. Wimbo huo ulichomolewa …
Yemi Alade Na Gode Video Ya Kiswahili
Wimbo wa “Na Gode” wa mwimbaji maarufu kutoka Nigeria Yemi Alade umekua ukitamba sana hapa nchini, na mwimbaji huyo ametoa video ya wimbo huo ambayo unaweza kuiona hapa chini.
Chama cha Karate Kilimanjaro Chaipigia Magoti Serikali
Vero Ignatus – Moshi Kilimanjaro CHAMA cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro wanaiomba serikali kutupia macho kwenye mchezo huo kwani imekuwa ikiwasahau ukizingatia mchezo huo ni michezo kama ulivyo mingine na kwamba mchezo huo umekuwa ukifundishwa pia katika majeshi mbalimbali hapa nchini. Hayo yamesemwa nakapteni wa timu na katibu msaidizi wa chama cha Katrate mkoa wa Kilimanjaro bwana Wembo Hamisi katika viwanja …