TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa, wanamuziki wa kundi la 5 star wamepata ajali mbaya eneo la Mikumi Morogoro na watu watano akiwemo muimbaji maarufu wa kundi hilo Issa Kijoti wamefariki dunia. Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wanamuziki wa kundi la taarabu la 5 Star, kugongana uso kwa uso na roli la mbao, wakati …
Mtanzania Flaviana Matata atwaa tuzo ya mwaka
Flaviana Matata, Mtanzania ambaye amekuwa akitengeneza vichwa vya habari katika majariba mbalimbali ya masuala ya ubunifu duniani, ameendelea kuing’arisha Tanzania katika masuala ya mitindo baada ya kutwaa tuzo ya Mwanamitindo bora wa mwaka huko nchini Nigeria. Tuzo hizo zilizotolewa na jarida maarufu la mitindo la Arize Magazine la nchini Nigeria, zilishuhusia Klûk CGDT, akitwaa tuzo ya mbunifu bora wa mwaka, …