Umati wa watu na mashabiki wa SERENGETI FIESTA wakishangweka katika tamasha hilo ndani ya viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam jana. Wasanii kibao walitumbuiza katika tamasha hilo linaloendelea kupata umaarufu kila uchao. Msanii wa miondoko ya bongo fleva, Linex kutoka jijini Mwanza akiwaburudisha mashabiki lukuki waliojitokeza kuhudhuria tamasha la mwendelezo wa msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta lililofanyika jana …
Loveness ndie Vodacom Miss Kanda ya Mashariki 2011
Vodacom Miss Eastern Zone 2011, Loveness Flavian (katikati) akipunga mkono akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Asha Saleh (kushoto) na Mariaclara Mathayo aliyeshika nafasi ya tatu, baada ya warembo hawa kutangazwa washindi wa shindano hilo. Loveness aliwashinda warembo wengine 10.Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni katika shindano la Vodacom Miss Kanda ya Mashariki, iliyofanyika mjini Morogoro …
Chaka Khan atembelea Clouds FM Tanzania
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akimkalibisha mgeni wake, Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Marekani, Chaka Khan alipotembelea ofisi hizo Dar es Salaam. Mwanamuziki huyo anatarajia kufanya onesho lake kesho (Julai 23) ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza, kwa udhamini mkubwa wa Club E.
‘FFU’ bendi waja na zawadi ya uhuru wa Tanzania
Kasha la wimbo wa bongo tambarare kama linavyoonekana pichani BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya, Ngoma Africa Band, aka ‘FFU’ imeanza shamra shamra za kusherehekea miaka 5O ya uhuru wa Tanzania mapema baada ya kutoa kibao chao kipya kinachojulikana kama Bongo Tambarare. Ngoma Africa band wamestua ulimwengu kwa kurusha hewani wimbo huo mpya uliobeba jina la “Bongo Tambarare” …
Miss utalii Tanzania 2011/12 kuzinduliwa Dodoma
Mhifadhi katika Hifadhi ya Tarangire, Beatrice Kessy (kulia) akifafanua jambo kwa washiriki Miss Utalii Tanzania 2011, katika ziara yao. BAADA ya kukamilisha uundaji mfumo mpya wa uongozi na uteuzi wa wakurugenzi 60 wa kamati ya Taifa hadi Wilaya wa Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation, yenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha …