T-Moto kuwang’alisha mashabiki kwa pamba, waingia studio kukamilisha kitu!

KUNDI jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) linalotarajia kuzinduliwa Oktoba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, limezindua mavazi yake rasmi kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wake siku ya uzinduzi. Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto Blogspot, Mkurugenzi wa Kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa wameamua kuandaa Tisheti kwa ajili ya wanaume na Vitop vya Kidada, zenye Nembo ya …

T-MOTO MODERN TAARAB YATUA DAR KUFYATUA SITA MPYA

KUNDI jipya la muziki wa taarab la Tanzania Moto Modern Taarab (T-Moto) limetua jijini Dar es Salaam leo asubuhi kutoka mfichoni katika Visiwa vya Zanzibar, lililokuwa limejichimbia kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wake uliosogezwa mbele hadi Oktoba 28 mwaka huu. Kundi hilo limewasili jijini baada ya kusitisha mazozi yake kwa muda kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa Meli …

Happy Birthday Kamanda yetu Ras Makunja wa ‘FFU’!

LEO Septemba 19, 2011 ni siku ya kuzaliwa mwanamuziki, Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja, mtunzi, mwimbaji na kiongozi wa bendi maarufu “Ngoma Africa band” aka FFU, yenye makao yake nchini Ujerumani. Kamanda Ras Makunja ambaye ni msanii nguli alizaliwa Katikati ya Jiji la Dar es Salaama Septemba 19. Ni mtoto wa kiume wa Jumanne Saleh Makunja (RIP) na Bi. …

Mapacha 3 wapagaisha Mashabiki Sin Cirro

KUNDI machachari la Bendi ya Mapacha Watatu linaloundwa na wanamuziki wanaovuma na nyota, yaani Halid Chokoraa, Kalala Junior pamoja na Jese Mara, jana waliwapagawisha mashabiki wao ndani ya Ukumbi wa Sun Cirro walipokuwa wakifanya unesho lao. Kwa mujibu wea mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo ameuambia mtandao huu kuwa kwa sasa wataendelea kutumbuiza ndani ya ‘Night Club’ hiyo ya kisasa …