Mpambano wa Matumla Osward hakuna mbabe

MPAMBANO kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ umemalizika jana jijini Dar es Salaam huku mabondia hao wakitoshana nguvu. Katika pambano hilo lililokuwa na ushindani mkubwa lilimalizika huku mabondia wote wakiibuka na pointi 99 kwa 99, hivyo majaji kulazimika kutoa droo kwa wababe hao.

Leo ni leo, nani mbabe kati ya Maneno Osward na Rashid Matumla

Mratibu wa pambano la Ngumi za kulipwa, Shabani Adios ‘Mwayamwaya'(katikati), akiwashuudia mabondia, Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ kushoto na Rashidi Matumla ‘Snake Man’, wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito leo, kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Helnken Mtoni KIjichi, Dar es Salaam siku ya X-Smas. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Dk Nchimbi atoa siku 75 kusakwa vazi la taifa

Na Beatrice Mlyansi na Benjamin Sawe WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi ameitaka kamati mpya ya kubuni vazi la taifa kukamilisha mchakato wa kupata vazi hilo ndani siku 75 ili liweze kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri kwa uamuzi zaidi. Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kamati hiyo, Waziri Nchimbi amesema kazi ya …

Mabondia Matumla na Oswald wapima vipimo

Na Mwandishi Wetu MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa, wamepima uzito na kukutwa wapo fiti kiafya. Pambano hilo la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam. Daktari wa mchezo wa ngumi nchini, Charles Kilaga, …

Kambi ya Ngumi Ilala kumuandaa bondia Ubwa Salum

KAMBI ya Mchezo wa Ngumi ya Mkoa wa Kimichezo wa Ilala, Dar es Salaam, inamuandaa bondia Ubwa Salum kwa ajili ya pambano lake dhidi ya bondia Mustafa Dotto, litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu. Akizungumza jana Dar es Salaam Kocha Msaidizi wa Kambi Ilala, Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema pambano hilo litakuwa kati ya mapambano yatakayotangulia katika pambano kali linalowakutanisha mabondia …