MSANII nyota wa muziki wa Kizazi kipya nchini Naseeb Abdul a.k.a Diamond na wenzake jana mjini Iringa amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya sh. 50.000 kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari mkoani Iringa Francis Godwin. Godwin ambaye pia ni mmiliki wa Blog ya Francis Godwin, hajaridhika na hukumu hiyo na tayari …
Maneno Osward kuzichapa tena na Rashid Matumla
Na Mwandishi Wetu MAANDALIZI ya pambano lisilo la ubingwa kati ya mabondia Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa kupigwa Februari 25 mwaka huu yanaendelea vizuri. Promota wa mpambano huo Issa Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99 Hata hivyo Oswald aliwalalamikia …
Bondia Karama kupokonywa ubingwa wa dunia
Na Mwandishi Wetu BONDIA Karama Nyilawila huenda akanyang’anywa Ubingwa wa Dunia unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Ulimwenguni (WBF) endapo atazipiga na bondia Francis Cheka. Taarifa ambazo zimetolewa na viongozi wa Shirikisho la ngumu nchini, zinasema Nyilawila atapokonywa ubingwa alionao endapo atang’ang’ania kuzipiga na Cheka kabla ya pambano lake la WBF linalotarajiwa kufanyika Februari 11, 2012. Bondia Nyilawila alitaka kupanda uringoni …
Bondia Super ‘D’ ajivunia mafanikio 2011
Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila ‘Super D’ na kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti ya Mkoa wa Ilala kimichezo amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata katika mchezo wa ngumi kipindi cha mwaka 2011. Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam Super ‘D’ alisema moja ya mafanikio hayo ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na …
Demba Ba achaguliwa kikosi cha Senegal
Senegal imetaja kikosi chake imara cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, huku kikiongozwa na mpachika mabao hatari katika Ligi Kuu ya Kandanda ya England, Demba Ba. Mfungaji hodari msimu uliopita katika Ligi ya Ufaransa Moussa Sow n mshambuliaji wa klabu ya Freiburg Papiss Demba Cisse pia wamo katika kikosi hicho. Simba hao …