Whitney Houston afariki dunia

MWANAMUZIKI maarufu nchini Marekani, Whitney Houston amefariki dunia. Houston ambaye pia aliwahi kuwa mcheza filamu na mwanamziki aliyefanikiwa amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48. Msemaji na mwandishi wa mwanamuziki huyo, Kristen Foster amekiambia chombo kimoja cha habari kuwa ni kweli Houston amefariki dunia japokuwa ajafafanua sababu za kifo chake. Magari sita ya polisi huku yakiwa yamewasha vimulimuli kuashiria …

Asha Baraka aanzisha taasisi ya kuvumbua vipaji vya ‘dansi’

MKURUGENZI wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, ameanzisha taasisi ya kuvumbua vipaji itakayojulikana kwa jina la Twanga Academia. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kwamba, Twanga Academia tayari imenunua vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 100 kwa ajili ya kuanzia katika taasisi hiyo. Amesema ili kupata vijana wa kuanza mafunzo …

Barnaba kurekodi na Fally Ipupa Ufaransa

MSANII mahiri wa miondoko ya Bongo fleva Elias Barnabas ‘Barnaba’, anataraia kuondoka nchini Machi 28, mwaka huu kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kurekodi kibao chake kipya kiitwacho ‘Tuachane kwa Wema, ambacho atamshirikisha mwanamuziki nyota wa muziki wa Dansi Fally Ipupa. Akizungumza na Blog ya Sufianimafoto, Barnaba, alisema maandalizi yote ya safari hiyo yamekamilika na tayari amekwishapewa tarehe ya kazi …

Bondia Mohamed kutetea ubingwa na Mkalekwa

Na Mwandishi Wetu BINGWA wa mkanda unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Abdalah Mohamed ‘Prins Naseem’ atapanda ulingoni Februari 24 kutetea mkanda wake kwa kuzichapa na bondia Salehe Mkalekwa. Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa na uzito wa kg 57 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo …