Mwigizaji Tony Burton Afariki Dunia Kifo chake ni Utata Mtupu

Tony Burton aliyeshiriki katika filamu sita za Rocky dhidi ya Sylvester Stallone amefariki akiwa na umri wa miaka 78. Kiini cha kifo chake bado hakijulikani ,lakini dadaake ,Loretta Kelly amesema kuwa amekuwa akienda hospitalini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Ameongozea kuwa hajapata utambuzi wa ugonjwa wake katika wakati huo na kwamba hali yake ya afya ilikuwa imezorota hali ya …

Sanjay Dutt Asamehewa Kifungo cha Miaka Mitano Jela

Nyota wa filamu za Bollywood Sanjay Dutt ameachiliwa kutoka jela katika mji wa magharibi wa Pune nchini India. Dutt mwenye umri wa miaka 56 alihukumiwa kifungo jela kufuatia makosa ya kumiliki silaha inayohusishwa na mlipuko wa 1993 mjini Mumbai ambapo takriban watu 257 waliuawa na wengine 713 kujeruhiwa. Alipatikana na hatia ya kununua silaha hiyo kutoka kwa walipuaji ,lakini akasema …

Duuu Hii Kali Kumbe Nywele Nazo ni Dili, Nywele za Msanii Zauzwa Dola 35,000

Mjini kila kitu kina thamani yaani ukikihitaji lazima utoe hela, sikia hii, Shungi la nywele ya msanii nguli wa muziki chapa Rock na muanzilishi wa kundi la ”The Beatles” John Lennon aliyeaga dunia miaka 36 iliyopita imeuzwa kwa dola elfu thelathini na tano ($ 35,000) katika mnada mmoja huko Marekani Kinyozi wa Muimbaji huyo maarufu kote duniani alificha shungi la …

Kylie Ajitangazia Kuwa Mchumba wake ni Mchekeshaji Joshua

Mwanamuziki Kylie Minogue ametangaza kuwa yeye ni mchumba wa Joshua Sasse. Baada ya wiki kadhaa za uvumi,wawili hao wametoa tangazo rasmi kwa kuweka notisi katika gazeti la Daily Telegraph nchini Uingereza. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 47 amekuwa akionekana na nyota huyo wa filamu nchini Uingereza kwa kipindi cha miezi sita. Inadaiwa huenda nyota huyo wa filamu alianzisha mjadala …

Pata Picha 19 za Vituko Michezo ya Simba na Yanga Zilizopita

Mashabiki wa Simba wakiwa Wamebeba Mfano wa Jeneza katika mchezo wao dhidi ya watani wao Yanga ambapo Timu ya SIMBA iliibuka na ushindi baada ya kuichapa timu ya YANGA bao 2 huku timu ya Yanga wakiambulia kuondoka na maumivu ya kushindwa kufurukuta kwa bao hata moja. Mashabiki wa Yanga wakiwa na mfano wa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya …