Cheka na Maugo waoneshwa gari watakaloligombea

Na Mwandishi Wetu WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameoneshwa rasmi gari watakalolishindania ifikapo Aprili 28 mwaka huu katika Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam. Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa …

Mama Kipingu atembelea Timu ya ngumi ya Taifa

Na Mwandishi Wetu, Kihaba Pwani MWAKILISHI wa Wanawake na Maendeleo ya Vijana, Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena’ Mama Kanari Kipingu’ ametembelea kambi ya timu ya ngumi ya Taifa na kuwaasa wawe makini wanapokwenda kwenye michuano ya kufuzu mashindano ya Olimpiki. Akizungumza na mabondia hao kambini kwao Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani jana,’ Mama Kanari …

Ngoma Africa Band watoka na Uhuru wa Habari

KWA kawaida wanahabari na vyombo vyao ndio wanarusha hewani habari za matukio mbalimbali pamoja wasanii na burudani zao kwa jamii, lakini bendi maarufu Ngoma Africa a.k.a FFU imewakumbuka wana habari na vyombo vyao. FFU imetoa hewani song jipya la “Uhuru wa habari”. Wimbo huo mpya mtunzi wake Kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na kijana Christian Bakotessa a.k.a Chris-B, ambaye …

Mama yake Kanumba atoa wosia kwa SHIWATA

Na Peter Mwenda MAMA Mzazi wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba amewataka wasanii wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuendeleza ushirikiano alioacha mwanae. Akizungumza katika ibada ya kumuombea mwanae iliyoandaliwa na M (SHIWATA) leo Dar es Salaam, Mama Kanumba alisema amefarijika kuona wasanii wanaendelea kumuombea mwanae kila kona ya nchi. “Nawashukuru SHIWATA kwa moyo wa ipendo …

Super ‘D’ aanzisha programu kutafuta mabondia Bora

Na Mwandishi Wetu KOCHA wa Kambi ya Ngumi ya Mkoa wa Ilala Kimichezo, Rajabu Mhamila, ‘Super D’, ameanzisha programu maalumu ya kuwafanyisha mazoezi mazito mabondia wake. Ameamua kuanzisha programu hiyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwa na pumzi na nguvu kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani. Akizungumza leo, Kocha huyo alisema kuwa mabondia wake watashiriki katika mashindano ya 10 …

Diamond ang’ara tena Tuzo za Kili 2012

MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa Kizazi kipya, Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond ameibuka tena kinara wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro (KTMA) baada ya kujishindia tuzo tatu tofauti kwa mwaka 2012. Diamond ameshinda tuzo hizo usiku huu katika Mkumbi wa Mlimani City baada ya kuibuka na tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Kiume, Mtunzi Bora wa Nyimbo na msanii …