Pumzika kwa amani Magoma Shabani

BONDIA wa kimataifa na bingwa wa dunia wa WBU uzani wa flyweight MAGOMA SHABAN amefariki jana saa mbili na nusu usiku katika hospital ya Bombo mjini Tanga anazikwa leo tarehe 1/6/2012 saa kumi nyumbani kwao MABOVU KWAKAHEZA mjini Tanga. katika uhai wake magoma Shaaban alikuwa bondia mahiri sana na aliweza kuwa katika timu ya taifa na kushiriki mashindano mengi mbalimbali …

Stars yawasili Abdjan, Kim ajitetea mechi itakuwa ngumu

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan (Mei 31 mwaka huu) mchana huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu. Stars yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu. Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast …

Meneja wa Twanga Pepeta aikimbia bendi, aenda Mashujaa

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Meneja Masoko wa Bendi maarufu na nguli ya African Stars Wana wa ‘Twanga na kupepeta’, Martine Sospeter jana ametangaza rasmi kujiunga na Bendi ya Mashujaa. Akizungumza Dar es Salaam jana katika mkutano na waandishi wa habari Sospeter, alisema maamuzi hayo yamekuja baada ya kuona hakutendewa haki na mwajili wake katika bendi hiyo. Alisema majuzi usiku alishangazwa …

Makocha 35 Copa Cocacola kushiriki semina ya FIFA

MAKOCHA 35 wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushiriki semina ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola. Semina hiyo itafanyika kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 4-9 mwaka huu chini ya mkufunzi kutoka FIFA, Ulric Mathiot. Makocha hao wanatakiwa kuripoti Juni 3 …