Baadhi ya Wanamuziki wa SKYLIGHT BAND wakishambulia Jukwaa mwishoni mwa wiki katika show ya kukata na shoka kwenye kiota chenye upepo mwanana cha THAI VILLAGE Masaki jijini Dar es Salaam. Pichani ni Rappa Sam Machozi akisindikizwa na Wenzake Aneth Kushaba AK 47 pamoja na SONY MASAMBA. Sam Machozi kazini. Hapa unapata kila kitu Style zote za muziki kuanzia Dancehall, Reggae, …
Mahoja Awatio Hofu Namibia
MTANZANIA Rajabu Maoja amelitingisha jiji la Windhoek, nchini Namibia alipoingia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako. Maoja aliingia kwa mbemwe za aina yake baada ya kukataa kukumbatiana na wenyeji wake ambao walikuwa na shauku ya kumkumbatia. Akiwa na sura ya kujiamini huku akitembea kibabe Mtanzania Maoja alionyesha nia ya kuuchukua mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara …
Maonesho ya Sarakasi yaendelea kurindima New World Cinema Dar
“Karibuni watanzania wote muone sarakasi na utamaduni wa kitanzania” Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya ‘Mama Africa Circus’. Picha Juu na Chini ni baadhi ya wadau walioshiriki maonyesho hayo wakifurahia.
Mchakato wa Uchaguzi wa Viongozi TAFCA Waanza
MCHAKATO wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka …