Mwanamuziki Rick Ross akiwatumbuiza umati wa wananchi walioshiriki Serengeti Fiesta 2012 jijini Dar es Salaam ndani ya viwanja vya Leaders Club. Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club, wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima. Mkali mwingine wa …
Serengeti Fiesta 2012, Dar es Salaam Yawaka Moto!
Wasanii wa kundi la Wanaume TMK, likiongozwa na Themba sambamba na Chege Chigunda wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya Lidaz Club, Kinondoni jijini Dar. uwanja wa Lidaz Club hapatoshi kabisa usiku huu. Nyomi la Watu ile balaa usiku huu. Wasanii wa kikundi cha Makomando kutoka THT wakionesha umahiri wao …
Msanii Rick Ross wa Marekani Atua Dar Tayari kwa Serengeti Fiesta 2012
Rick Ross akitoa salamu ya salut kwa washabiki wake waliojitokeza usiku huu (hawapo pichani) kumlaki. Operesheni Meneja wa Prime Time Promotions, Balozi Kindamba akiwaongoza wageni wake kuelekea kwenye gari tayari pamoja na msanii wa kimataifa Rick Ross na akiwa na baadhi wanamuziki wenzake aliombatana nao. Rick Ross akiingia ndani ya mchuma. Rick Ross akiondoka na mchuma wake kuelekea hotelini usiku …
Africa Magic, Multichoice Yaandaa Tuzo kwa Waigizaji na Watengenezaji Filamu
Bi. Risper Muthamia amesema kuwa Filamu zote zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni na mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) zinaweza kuwasilishwa kuwania tuzo hizo iwapo zilitengenezwa na kurushwa hewani au kuonyeshwa hadharani katika kipindi cha kati ya May 1, 2011 hadi April 30, 2012. Aidha amefafanua kuwa Filamu au vipindi vitakavyoshiriki katika tuzo hizo viwe ni katika lugha ama ya …
Promota wa Ngumi Kutoka Misri Atembelea Tanzania
PROMOTA maarufu wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Misri, Richard Nwoba kutoka kampuni ya “Louaa Boxing Promotions” ametembelea ofisi za IBF zilizoko jijini Dar-es-Salaam ili kuangalia uwezekano wa kupromoti mapambano ya ngumi katika Ukanda wa Mashariki na Kati. Nwoba akiwa nchini Tanzania alikutana na Rais wa IBF Afrika, Mashariki na Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi , Onesmo Alfred McBride …
King Class Mawe Afuliwa Kumkabili Bondia Segu
BONDIA Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ yupo katika mazoezi makali kwa ajili ya mpambano wake na bondia Jonas Segu litakalofanyika Oktoba 14, 2012 ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila …