Bondia Francis Cheka Kupigana na Udiadia Mwahia wa DRC-Congo

Na Mwandishi Wetu BONDIA maarufu nchini Tanzania, Francis Cheka anatarajia kupanda uringoni kuvaana na bondia Udiadia Mwahia kutoka nchini DRC Kongo ikiwa ni pambano la kugombea mkanda wa Ubingwa wa IBF barani Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi. Mabondia hao wanatarajia kukutana katika mpambano wa kwanza tangu Mkoa wa Arusha kutangazwa Jiji na pambano lao linatarajia kufanyika katika …

Nassibu Ramadhani Kuzichapa na Fransic Miyayusho Kugombea Ubingwa wa WBF

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho, mpambano utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mohamed Bawazir alisema wameamua kuwakutanisha mabondia hao baada ya kuona kila mmoja anamtambia bondia mwenzake. Alisema mpambano huo utamaliza ubishi na kujua nani …

Kituo cha Tanzania Mitindo House na Miaka Mitano Tangu Kuanzishwa

Tanzania Mitindo House imefanya sherehe ya kusheherekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kula chakula cha mchana na watoto yatima kutoka ‘Malaika Orphanage Center’ na ‘Umraa Orphanage Center’ katika kituo chao cha kuchezea watoto yatima kilichopomanispaa ya Temeke.Pichani Juu na Chini ni Watoto wakicheza michezo mbalimbali katika sehemu maalum ya Tanzania MitindoHouse Fun Centre. Sherehe hizo zimedhaminiwa nan KIONDO COMMUNICATIONS INTERNATIONAL, …

Mabondia wa Timu ya Taifa ya Ngumi Tanzania Walivyo Kula Kichapo

MABONDIA wa ngumi za Ridhaa wa Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita wamechezea kichapo baada ya kupigwa michezo minne kati ya mitano iliyochezwa na mabondia toka Zambia kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo. Mapambano hayo ambayo yalikuwa ni ya kirafiki ya kimataifa kati ya nchi hizo mbili Tanzania na Zambia, yanayotambuliwa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Duniani (AIBA) yaliokuwa na raundi …

Mabondia Mazola na Juma Kuzichapa Jumapili

BONDIA Baina Mazola toka katika gym ya Mzazi Respect ya Mabibo atazipiga na mtoto wa Mwananyamala, Mwaite Juma katika pambano lisilo la ubingwa la raundi nane. Pambano hilo litafanyika Jumapili ya Novemba 18, 2012 katika Ukumbi wa DID Mabibo, ambalo ni maalumu kuwania kucheza ubingwa huo. Mshindi wa pambano hilo atakuwa na nafasi ya kucheza pambano la ubingwa na bondia …

Huyu Ndiye Bingwa wa Michuano ya JOHNNIE WALKER Waitara 2012

Mshindi wa jumla wa mashindano ya kuwania kombe la Johnnie Walker Waitara 2012 Sudson Manatsa akinyanyua juu vikombe vyake viwili alivyoshinda wakati wa Mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake kikali cha Johnnie Walker.   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya …