Wapiga vyombo wa SKYLIGHT BAND wakiwapa raha mashabiki. Kifaa kipya cha SKYLIGHT BAND kikicharaza Gitaa. Aneth Kushaba AK47 katika hisia kali. Kijana SAM wa SKYLIGHT BAND akiimbia kwa hisia kali. Shabiki akionekana kukunwa na sauti za warembo wa SKYLIGHT BAND. Pichani Juu na Chini Mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakisakata mduara kwa raha zao. Kuna walioingia kati na kumwaga radhi kama …
George Haule Aibuka na Mwamba ni Yesu
MWIMBAJI chipukizi wa Nyimbo za Injili, George Haule, amepakua Albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Mwamba ni Yesu na sasa ipo mtaani. Akizungumza na Father Kidevu Blog, mtumishi huyo wa Mungu amesema albam yake ina nyimbo 8 lakini Mwamba ni Yesu ndio uliyobeba jina la albam yake hiyo ya kwanza. Haule amewaomba watanzania na wapenzi wa nyimbo za …
Wimbo wa “Mama Kimwaga” wa Ngoma Africa Band Wazua Balaa
Bremen, Ujerumani KATIKA hali ya utatanishi kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja wa FFU amejikuta akipewa mashaka ya maisha na mwanamama moja kisa wimbo “Mama Kimwaga” ! ambao takribani mwezi mzima wimbo huo na nyingine za bendi zimekuwa zikipigwa mara kwa mara na kituo cha Radio Funk haus, inayorusha matangazo mjini Bremen, Ujerumani. Mwanamama moja ambaye aliguswa sana …
Bendi ya Mashujaa Musica Kufanya Show na JB Mpiana Dar
KAMPUNI ya QS ya jijini inatarajia kumleta nchini mwanamuziki nguli wa Jahmuri ya Kidemokrais ya Congo, JB Mpiana wa bendi ya Wenge BCBG katika uzindizi wa bendi ya Mashujaa Musica ya jijini unaotarajia kufanyika katika viwanja vya Leaders November 30 mwaka huu. Bendi hiyo ya Mashujaa inatarajiwa kuzindua albam yao ya ‘Risasi Kidole’ yenye nyimbo sita. Burudani zingine zitakazokuwepo siku …
Bondia King Class Mawe Aendelea Kujifua Kumkabili Said Mundi
Bondia Ibrahimu Class ‘King Class mawe’ akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Mohamed Hemedi ‘Kadogo Ninja’ wakati wa mazoezi yao yanayoendelea Katika Kambi ya Ilala Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. Picha na Super d blog.