Bingwa wa Pan-African Guinness Football Challenge Kujulikana Kesho

JUMATANO iliyopita tarehe 19 Mei 2013 kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, timu pinzani kutoka barani Afrika zilipambana kushindania nafasi mbili za fainali ya mashindano ya Pan-African Guinness Football Challenge. Walikuwa ni kutoka Ghana Emanuel Kofi Okarku na Isaac Aryee ambao kwa mara nyingine walianikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness. Wakenya katika jezi …

Iddy Kipandu Kuzichapa na Bahati Mwafyela

Na Mwandishi Wetu BONDIA Iddy Kipandu ‘Iddy Bonge’ yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya Sikukuu ya Idi pili jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Friends Corner Manzese. Akizungumzia maandalizi ya mpambano mtayarishaji wa mpambano, Waziri Rosta amesema pambano hilo la uzito wa juu ambalo limekuwa gumzo kwa mashabiki wa mchezo yanakwenda …

Salshia Isidore Atwaa Taji la Redd’s Miss Geita 2013

Na Father Kidevu Blog, Geita MREMBO Salshia Isidore amechaguliwa kuwa Redd’s Miss Geita 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 12 katika shindano lililifanyika Jumamosi Juni 1,  kwenye ukumbi wa Desire uliopo mjini Geita. Wengine walioingia nafasi ya tatu bora ni pamoja na Nurieth Rashid aliyeshika nafasi ya tatu na Stella Magerezi alishika nafasi ya pili. Katika shindano hilo lililosindikizwa na burudani safi kutoka kwa msanii Baby Madaha na …

Kinachodaiwa Kumuua Mangwea Hiki Hapa

WAKATI mazishi ya mwanamuziki marehemu Albert Mangwea (28) maarufu kama `Ngwair’ yakitarajiwa kufanyika mjini Morogoro, maeneo ya Kihonda baada ya mwili kuwasili nchini, hospitali iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa za kulevya kupita kiasi ndivyo vilivyomuua. Mwili wa mwanamuziki huyo, ambaye alitamba kwenye miaka ya 2000 na wimbo wa `Mikasi’, unatazamiwa kuletwa kesho nchini na kuagwa Jumamosi kabla ya …