Hatimaye Kenya Yatwaa Ubingwa wa Pan-African Guinness Football Challenge

*Afrika Mashariki zachua vikali na Afrika Magharibi kuwania ushindi HAIJAWAHI kutokea mpambano mkali katika Guinness Football Challenge kama uliooneshwa jana katika fainali za michuano ya Pan-African Guinness Football Challenge kupitia vituo vya televisheni za ITV na Clouds TV. Fainaili ilikuwa na ushindani mkubwa ambapo timu mbili kutoka Afrika Mashariki na nyingine mbili kutoka Afrika Magharibi zilichuana vikali kila timu zikiwania …

Mafuriko Yavamia Tamasha Ujerumani, Wasanii Waponea Chupu Chupu

JUMAMOSI ya Juni Mosi 2013, katika viwanja vya maonesho ya Wurzburg Festival, ilikuwa ni majonzi na simanzi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yalisababisha hasara kubwa na kuvunjwa kwa tamasha hilo lililokuwa likisherekea maadhimisho ya miaka 25. Habari za uhakika zimevuja kuwa vikosi vya zimamoto na wanausalama viliingiwa na mashaka baada ya wasanii wa Ngoma Africa Band a.k.a FFU, …

Barrick Gold Mining Watoa Milioni 10 Kudhamini Redd’s Miss Mara

  Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd’s Miss Mara 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jana ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

Msanii Khadija Kopa Afiwa na Mumewe

Khadija Kopa Afiwa na Mumewe MSANII maarufu wa muziki wa taarab, Khadija Omar Kopa amefiwa na mume wake, Jafari Ali Yussuf aliyekuwa mgonjwa. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba mara tu baada ya Khadija Kopa kupewa taarifa hizo alipokuwa kwenye chumba maalumu cha kupumzikia wageni ndani ya Uwanja wa Ndege wa Mpanda aliishiwa nguvu na kuanza …

BFT Kufanya Uchaguzi Mkuu Julai 7

Yah: Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) kwa kulingana na Katiba yake, sheria na kanuni za Baraza la Michezo la Taifa (BMT)linatarajia kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa kuongoza Shirikisho kwa kipindi cha miaka mine ijayo. Uchaguzi huo unatarajia kufanyika tarehe 07/07/2013 jijini Mwanza, sambamba na mashindano ya majiji. Nafasi zitakazogombewa ni …

Zanzibar International Film Festival Kuanza Juni 29

Na Genofeva Matemu na Lorietha Laurence – MAELEZO MAONESHO ya filamu, utamaduni, kazi za mikono na burudani yajulikanayo kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF) yanatarajiwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 29 Juni hadi tarehe 7 Julai mwaka huu. Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF Profesa Martin Mhando alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo la …