Wawakilishi wa Tanzania Mashindano ya Guinness Football Challenge Washerehekea..!

BAADA ya kumalizika kwa mashindano ya Guinness Football Challenge yaliyokuwa yakiendeshwa na Kupitia kipindi maarufu cha Guinness Football Challenge TV Show, hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo jana wamefanyiwa sherehe fupi katika Ukumbi wa Savannah Lounge Jijini Dar es Salaam na waandaji na wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwapongeza kwa hatua waliyofikia. Yaliyokuwa yakifanyika …

Redds Miss Kinondoni 2013 Wafanya Harambee Kusaidia Hospitali Mwananyamala

Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa  Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina ambapo warembo hao walitembelea wodi za akina mama na kufanya usafi. Pamoja na harambee kulizinduliwa …

Redd’s Miss Kinondoni 2013 Kufanyika Golden Tulip Juni 21

Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira. Ambapo mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye …

Warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 Watembelea Mradi wa DART

Bango la ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) lililoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Msimamizi wa mradi huo, akitoa maelezo kwa warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 ambao waliambatana na Madiwani wa Viti Maalum kutembelea ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka zilizoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Ziara ya warembo hao ilikuwa na nia ya …