BANDI ya Ngoma Africa a.k.a FFU ya ughaibuni, bendi maarufu yenye ngome yake Ujerumani, chini ya uongozi wa kamanda wao Ras Makunja, bendi hiyo imefanya kweli siku ya Jumapili ya Julai 28 katika maonesho ya Jambo Seeheim Festival, yaliyofanyika mjini Jugenheim-Seeheim, nchini Ujerumani kuliko ungua shoka mpini ukabaki. Ngoma Africa band ilianza kuwasha muziki mkali na kuwatia kiwewe washabiki waliokuwapo …
Mabondia Kambi ya Bigright Boxing Waendelea Kujifua
MABONDIA toka kambi ya Bigright Boxing ya Mwananyamala wapo kambini wakiendelea kujifua kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao ambao wanatarajia kuzichapa katika wakati tofauti na maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi. Mabondia hao ni Issa Omar anaetarajiwa kuzipiga katika Ukumbi wa Government Complex nchini Zambia na Pethias Chisonga wa Zambia chini ya uratibu wa Exodus Stable ya nchini humo. …
Mbondia Mtanzania Amtwanga M-Thailand kwa KO
BONDIA Mtanzania, Omari Kimweri ‘Lion Boy’ anaefanya shughuli zake nchini Australia amendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangia angie katika ngumi za kulipwa akiwa nchini humo. Bondia huyo ambaye anaitangaza vema nchi ya Tanzania Kimataifa ameahidi kuendelea kutoa vipigo kwa mabondia mbalimbali pindi …
Thomas Mashali ‘Awatusi’ Mabondia Wenzake
BONDIA Thomas Mashali amewatusi mabondia wenzake Mada Maugo na Kalama Nyilawila kwa kuwafananisha na midoli na kuwakebehi kuwa si chochote wala lolote kwake. Hatua hiyo ya Mashali inatokana na awali kupondwa na Maugo kuwa hana uwezo na ni heri akageukia biashara ya kuuza chapati, wakati Kalama akimkebehi kuwa ni kibonde wake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika chumba chake …
Msondo Ngoma Waingia Studio Kutoa Mpya
BENDI Kongwe ya Muziki wa dansi nchini Tanzania ya Msondo Ngoma imeingia Studio kurekodi nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika album moja. Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Bendi Hiyo, Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema kuwa bendi yake kwa sasa imeingia studio kukamilisha kurekodi nyimbo zao mpya ambazo zinatarajia kuvuta hisia ya wapenzi wa muziki nchini. Alizitaja nyimbo hizo kuwa …
Bondia Omari Kimweri Atamba Kushinda Pambano Lake
BONDIA Mtanzania, Omari Kimweri ‘Lion Boy’ anaechezea uzito wa light flyweight anaefanya shughuli zake nchini Australia anatarajia kupanda ulingoni mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya mpambano wake mwingine baada ya kuwatwanga mabondia kadhaa nchini humo. Akizungumzia pambano hilo, alisema ataendeleza wimbi la ushindi kwa kutoa vipigo kama alivyotoa kwa bondia Yodpichai Sithsaithong pamoja na Lookrak Kiatmungmee ambazo ndio mechi zake za mwisho kucheza …