Mratibu wa Mradi wa Tamasha la Fiesta 2016 kutokaTigo, Balla Shareeph (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya kuwataja washindi 16 Super Nyota Tigo Dar es Salaam leo. Kulia ni Mratibu wa shindano hilo, Nickson George na katikati ni Mshindi wa shindano, Galla Mligo ‘Galla Bway’ kutoka Dar es Salaam ambaye alizungumza kwa niaba ya washindi wote. Mratibu wa shindano hilo, Nickson …
Nape Amlilia Bondia ‘Thomas Mashali’
WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa pamoja na Chama cha Wanandondi nchini kufuatia kifo cha Bondia wa ngumi za kulipwa Bw. Christopher Fabian Mashale maarufu kama ‘Thomas Mashali’ kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 31/10/2016. Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko …
Bondia Mashali Apigwa hadi Kufa na Watu Wasijulikana
BONDIA Christopher Fabian Mashale maarufu ‘Francis Mashali’ amefariki dunia baada ya kupigwa na watu ambao bado hawajajulikana usiku wa kuamkia leo. Taarifa zinasema kwamba mwili wa mbabe huyo aliyezaliwa Septemba 9 mwaka 1989, mwili wake umekutwa maeneo ya Tabata ukiwa na dalili za kupigwa. Promoka Siraj Kaike amesema taarifa alizonazo ni kwamba mwili wa marehemu kwa sasa upo hospitali ya …
Ikungi Half Marathon Zafanyika Mkoani Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwapongeza washiriki waliomaliza kwa wastani mzuri wa muda, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu. Bi Zaibabu Ramadhani mwenye umri wa miaka 47 akiwasili Katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kumalizia kilomita 21. Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akisalimia na Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika …
Ujerumani Yachangia Milioni 12 Tamasha la Sauti za Busara
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.
Wabunifu mitindo waonesha mavazi uzinduzi duka la maharusi
Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang ‘Bang Magazine’, Emelda Mwamanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi ‘Precious Wedding House’ lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo pamoja na Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa (kulia). Uzinduzi huo uliofanyika Sinza …