UWANJA WA NDEGE DODOMA SASA KUTUMIKA SAA 24

    SERIKALI iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi wa kufunga Taa za kuongozea ndege ili kuruhusu Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuweza kutumika masaa 24. Akizungumza hayo mjini Dodoma mara baada ya kukagua Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light) zilizofungwa uwanjani hapo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa hatua hiyo …

SEKTA YA VIWANDA NCHINI NA ULIPAJI KODI YA MAPATO

CHEMBA ya Madini na Nishati (TCME) imetambua na kuguswa na taarifa zisizo sahihi kwamba kampuni zinazojihusisha na uchimbaji mkubwa wa madini zimekuwa zikifanya shughuli zake hapa nchini bila ya kulipa kodi ya mapato. Chemba hii ni muwakilishi wa makampuni wanachama waliorasimisha shughuli zao katika sekta ya madini kuanzia kampuni ndogo za utafiti wa madini hadi wachimbaji wakubwa na wa kati …

Wafanyabiashara Dar wanufaika na mafunzo ya kijasiliamali

              BENKI ya NMB imekutanisha wafanyabiashara zaidi ya 500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya wafanyabiashara wa NMB “NMB Business Club” kwa lengo la kutoa mafunzo mbalimbali ya biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao. Kundi hilo la NMB Business Club mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa …

Sekta Binafsi Kukutana na Rais Mkutano wa TNBC

WADAU wa Sekta binafsi nchini Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu. Mkutano huo wa ndani uliandaliwa na Taasisi ya Sekta binafsi nchini – TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu namna bora ya kuiwakilisha sekta binafsi katika …

NMB WAZUNGUMZA NA WATEJA WAO ZANZIBAR

    BENKI ya NMB kwa kupitia tawi lake la NMB Zanzibar imeandaa hafla na kuwakusanya wateja wake wadogo na wakati ambao ni wanachama wa klabu ya biashara ijulikanayo kama “NMB Business Club” ili waweze kuzungumza nao katika ufanikishaji wa biashara zao lakini pia kutoa mafunzo ya kibishara. Hafla hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na Meya wa Manispaa ya Mjini Zanzibar, …