Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango. Dk. Nchimbi amesema kuwa watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi chochote wakati inaleta pesa nyingi za …
Serikali Kutumbua Wahujumu wa TAZARA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambaye ataendelea kuisababishia hasara Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa kuendelea kuihujumu na kusababisha mamlaka kujiendesha kwa hasara. Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Tazara, kuangalia utendaji ambapo amebaini matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua stahiki. “Ninafahamu …
Wakulima Zaidi ya 60,000 Kunufaika na Mradi wa AMDT
Na.Vero Ignatus -Arusha. Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)imewataka wakulima kubadilisha kilimo kuwa biashara ,waondokane na kilimo cha kawaida na kuwa na kilimo cha kisasa na kufahamu kilimo mkataba. Hayo yamesemwa na meneja mradi Martin Mgallah alipokuwa katika maonyesho ya zana za kilimo Jijini Arusha na kusema kuwa wametenga zaidi ya dola za kimarekani milioni kumi …
RC Ataka Malighafi za Kilimo Kuuzwa kwa Gharama Ndogo!.
Imeelezwa kuwa teknolojia duni,rasilimali fedha,malighafi kuwa juu, uhaba wa mvua unaotokana na uharibifu wa mazingira ndio changamoto kubwa inayomkabili mkulima wa Tanzania kutofikia malengo ya kufanya kilimo biashara. hayo yamebainishwa na mkuu na mkoa wa arusha mrisho gambo aliyewakilishwa na mkuu wa wilaya ya arusha fabian daqarro kwenye maonyesho ya zana za kilimo yanayojulikana agritech expro Tanzania yamefunguliwa jijini arusha …
Dk Magufuli kuwa Mgeni Rasmi Siku ya Sheria Nchini
Benjamin Sawe -Maelezo. Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake …
Jaji Lubuva Akabidhi Taarifa ya Utendaji miaka 5 kwa Mwenyekiti Mpya
Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara baada ya kukabidhi taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Wajumbe wa …