Na Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U) Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa kukarabati meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha utendaji kazi wa kampuni hiyo. Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo Eng. Dkt. …
Rais Magufuli Akutana na Makamu Rais wa Benki ya AfDB
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 17 Februari, 2017 amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott ambaye yupo hapa nchini kwa mazungumzo na wataalamu na viongozi yenye lengo la kuboresha sekta ya nishati hususani uzalishaji wa umeme. Bw. Amadou …
UUNDP Yakutana na Kuzungumza na Wanafunzi wa Shule ya Wasichana Weruweru
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez (katikati) akiwa ameongozana na Mkurugenzi anayesimamia Mashirika ya Umoja wa Mataifa , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushi (kushoto) na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ya mkoani …
Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu Wasaidia Makazi ya Wazee Singida
NA MWANDISHI MAALUM MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu. Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali …
Sekta ya Uchukuzi Yaelekea Dodoma, Wamfuata Waziri Mkuu
Na Biseko Ibrahim WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka watumishi wa Wizara hiyo Sekta ya Uchukuzi kutumia vizuri fursa ya kuhamia Dodoma kwa kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na weledi. Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwaaga watumishi wa Sekta ya uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao wameondoka leo kuelekea mjini Dodoma. “Nawapongeza kwa kupata fursa …
Makonda Akabidhi Majina Mengine ya Watuhumiwa Dawa za Kulevya
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amekabidhi orodha nyingine ya watuhumiwa wa dawa za kulevya ili waweze kushughulikiwa na Mamlaka Mpya ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya. Makonda amekabidhi faili la majina hayo kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers William ambaye ameahidi kuendeleza moto ule ule wa mapambano ili kuhakikisha wanatokomeza biashara hiyo …