Bodaboda Arusha Waua Mtu Baada ya Kumfananisha

Na Vero Ignatus, Arusha MTU moja ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha, akidhaniwa kuwa ni mwizi wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha pikipiki hao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo (pichani juu) amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa majira ya saa saba mchana wananchi hao walimuona mtu …

Waziri Mbarawa Awataka TEMESA Kuongeza Ujuzi Utengenezaji wa Vivuko

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kushiriki kikamilifu shughuli za matengenezo ya vivuko ili kupata ujuzi wa ufungaji wa mifumo kutoka Kampuni zinazotengeneza vivuko vya Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuvko kipya cha MV Kazi, Bandarini jijini Dar …

Naibu Waziri Injinia Ngonyani Aridhishwa na Kasi ya Utendaji wa TBA

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ameupongeza Wakala wa Majengo Nchini (TBA), kwa jitihada wanazozifanya katika kuongeza mapato na kununua vifaa vipya na kisasa vitakavyowezesha wakala huo kumudu ujenzi wa miradi mingi mikubwa kwa wakati. Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa nyumba 851 ulioko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na mabweni …

Waziri Dk Tizeba Kufungua Kongamano la Sera za Kilimo

  Enles Mbegalo WAZIRI wa Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku  tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini Dar es Salaam. Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa  Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, …

Prof Waziri Mbarawa Uso kwa Uso na Bodi ya AfDB

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiomba Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika mkakati wake wa kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu. Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi ya AfDB waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Prof. Mbarawa ameishukuru benki hiyo kwa ushirikiano inaoipa Serikali ya …