BENKI ya NMB imekabidhi udhamini wa shilingi Milioni 50 kwa jeshi la polisi kwaajili ya kufanikisha mkutano mkuu wa jeshi la polisi unaoendelea mkoani Dodoma kwa siku tatu. Mkutano huo unajumuisha maafisa waandamizi wa polisi na makamanda wa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani. Udhamini huu unalenga kufanikisha mkutano huo wenye malengo ya kujadiri changamoto na mafanikio …
Waziri Mwigulu Awataka Askari Polisi Kutobambikia Kesi Raia
Mzee John Samwel Malecela akizungumza wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi. Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa …
PROF. MBARAWA: NEEMA YAJA WAFANYABIASHARA KANDA YA ZIWA
IMEELEZWA kuwa kukamilika kwa ukarabati wa meli ya MV Umoja kutarudisha huduma ya usafirishaji wa mizigo katika kanda ya ziwa kupitia bandari ya Kemondo iliyopo mkoani Kagera. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati akikagua Bandari hiyo kuangalia maendeleo yake, na kuitaka Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Shirika la Reli …
Wafanyakazi Halotel Kufanya Usafi wa Mazingira Nchi Nzima
KUELEKEA kuwepo kwa kampeni mbalimbali zinazolenga kuboresha usafi wa mazingira na miundombinu kumeendelea kuwaamsha wadau na taasisi mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada hizo, ambapo kampuni ya mawasiliano ya Halotel imezindua kampeni ya wafanyakazi wake kufanya usafi katika maeneo yote yanayozunguka minara iliyojengwa na kampuni hiyo. HALOGREEN, ndio jina la kampeni ambayo ina lengo la kuboresha mazingira yanayozunguka maeneo yaliyojengwa …
Makaburi 22 ya Watu Wenye Ualbino Tanzania Yafukuliwa
TANGU kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini Tanzania yamefukuliwa na watu wasiojulikana. Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba. …
Mbunge Ridhiwani, Madiwani Chalinze Waibana CHALIWASA
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Chalinze, wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) kwa kushindwa kusambaza maji ili kuondoa kero hiyo. Alisema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini unasuasua. Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani lililofanyika Lugoba. Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado …