KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa vyakula mbalimbali na vinywaji katika vituo vya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa ajili ya kusherekea Siku Kuu ya Pasaka. Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni nne umetolewa leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurejesha sehemu ya faida kwa …
Rais Magufuli Awalilia Askari Nane Waliouwawa na Majambazi Kibiti
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni tarehe 13 Aprili, 2017 katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi …
NMB washiriki kampeni kuhamasisha vijana uelewa masuala ya fedha
Na Mwandishi Wetu BENKI ya NMB imeshiriki kampeni zilizoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo UN- CDF zinazowakutanisha vijana pamoja na mashirika mbalimbali yanayofanya kazi kuwahusisha maendeleo ya vijana. Kampeni hizo ‘BankTheYouth’ zilizowakutanisha vijana na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili zimelenga kuhamasisha vijana nchini kupata uelewa wa masuala …
Rais Magufuli Mgeni Rasmi Uzinduzi Mabweni ya Wanafunzi UDSM
RAIS Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mabweni mapya ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 15 Aprili, 2017. Katika siku hiyo hiyo, Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba …
Dk Wilson Ngwale Apewa Uwenyekiti Bodi ya TBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania …