ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi. Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi. Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka …
TAMWA yajivunia kuwawezesha wanahabari 2470 kimafunzo
KILA ifikapo Mei 3 ya kila mwaka wanahabari na wadau wa vyombo vya habari ulimwenguni huadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Maadhimisho ya mwaka huu (2017) kitaifa nchini Tanzania yalifanyika mkoani Mwanza na kushirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari. Miongoni mwa hoja zilizoteka mijadala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa …
Wananchi Kijiji cha Uhambila Wajadili Utunzaji Maliasili na Vyanzo vya Maji
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano wa kijiji wa kujadili maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja Maliasili za kijiji hicho. Na Fredy Mgunda, Iringa WANANCHI wa Kijiji cha Uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji hicho. Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho Afisa mradi …
Siku ya kitaifa ya uelewa juu ya Albino kufanyika Dodoma Juni 13
Chama Cha Watu Wenye Ualbino Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi za Watu Wenye Ulemavu, mashirika mengine yasiyo ya kiserikali na wadau mbalimbali mwaka huu watafanya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa Juu ya Ualbino mjini Dodoma ambayo kilele chake ni tarehe 13 Juni. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri …
Rais Magufuli Aifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma, CDA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 15 Mei, 2017 ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na ameagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Mhe. Rais Magufuli ameivunja CDA kwa kutia saini hati ya Amri ya Rais ya …
Naibu Katibu CCM Zanzibar Awataka Viongozi Kufanya Kazi za Kijamii
Na Is-Haka Omar, Zanzibar WANANCHI visiwani vya Zanzibar wameshauriwa kuendeleza kwa vitendo Utamaduni wa uzalendo wa kusaidiana wakati wa maafa mbali mbali yanayotokea nchini bila kujadili tofauti za kisiasa na kidini. Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadala “Mabodi” mara baada ya ujenzi wa nyumba ya Balozi wa Nyumba kumi, Bi. …