TCU Yataka Wanaokwenda Kusoma Vyuo vya Nje Kuzingatia Vigezo

  TUME ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) imesema kuwa wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa kuangaliwa vigezo ambavyo vinahitajika. Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda …

DARAJA LA MAGARA KUANZA KUJENGWA MWEZI JULAI

    SERIKALI imesema ipo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayejenga Daraja la Magara lenye urefu wa Mita 84 katika barabara ya Mbuyu wa Mjerumani-Mbulu km 21 lililopo mkoani Manyara ambapo mkataba huo unatarajiwa kusainiwa mwezi Juni mwaka huu. Akizungumza hayo jana kwa wananchi wa Kijiji cha Mayoka, wilaya ya Babati, mkoani humo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi …

Manispaa ya Ilala Yatoa Cheti cha Shukrani kwa Mwananchi Kichangani

  Na Leonce Zimbandu MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha shukurani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani kata ya Majohe, Gabriel Macheho (pichani) baada ya kutambua mchango wake wakuhifadhi na kutunza rasilimali za umma.    Moja ya rasilimali hizo ni pamoja na kusimamia eneo la umma lisichukuliwe na kumilikiwa na watubinafsi, likiwamo eneo la machimbo ya mchanga lililokuwa likimilikiwa na Mbezi …

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Waelimsha Wadau

        MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini katika mikoa minne, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao. Akizungumza katika semina hiyo mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko Dkt. Francis Michael …

Ripoti ya Mchanga Yamng’oa Waziri Muhongo…!

            RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye. Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada …

CHATO WATAKIWA KUCHANGAMKIA KILIMO CHA MIHOGO CHENYE TIJA SOKO LA KIMATAIFA

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo …