KATIBU WA BUNGE ZIARANI GHANA

Katibu wa Bunge la Tanzania akiwa Mwenyekiti wa kikao cha Tathimini ya Maandalizi ya Mkutano wa kwanza wa Makatibu wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika nchini Ghana.

10 Wauawa kwenye Ghasia Mjini Arusha, Tanzania.

  Watu wasiopungua kumi wameripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA. Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa.

TIDO MHANDO ATEMWA TBC

Sadick Mtulya na Patricia Kimelemeta BAADA ya kufanya kazi nzuri ya kuboresha matangazo na uendeshaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), serikali imeamua kuachana na mkurugenzi wa chombo hicho, Tido Mhando baada ya mkataba wake kuisha, lakini mtangazaji huyo maarufu ameielezea uamuzi huo kuwa kuwa ni wa utata. Kuenguliwa kwake kumefanyika takriban miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi …